Simu za Android zashambuliwa na Gooligan; Angalia kama upo salama 😨

0
Sambaza

Imethibitika kwamba wadukuzi wamefanikiwa kuzishambulia simu karibu milioni moja za Android kwa kutumia kirusi cha Gooligan, kirusi hiki inasemekana huingia katika simu kupitia App zinazopatikana katika masoko yasiyo rasmi ya Apps.

gooligan android kirusi simu

Tayari simu milioni moja duniani kote zimethibitika kuathiriwa na Gooligan, katika hizo asilimia 57 zinapatikana katika bara la Asia 19% bara la Amerika na katika bara la Ulaya ni 9% Afrika nzima ni asilimia 19 ya simu zote za android ndio zimeathirika.

Kirusi hiki kinaingia katika simu baada ya mtumiaji kupakua na ku-install app kutoka katika soko lisilo rasmi( 3rd  party market) na baada ya kuingia katika simu ya mtumiaji app hizi huanza kuiba nywila ambazo unatumia katika kuingia katika mitandao mbalimbali hasa ya Google.

gooligan

Muonekano wa jinsi gani wadukuzi wanafanikisha shambulizi; hichi ndicho tulichoelezea

Tayari uchunguzi unaonesha kwamba kirusi hiki cha Gooligan kinapatikana katika app zaidi ya 80 ambazo zinapatikana katika masoko yasiyo rasmi, hii ni tishio hasa kwa sisi ambao tunatumia app hizi katika simu zetu.

SOMA PIA:  Ifahamu simu janja Tecno H5 kwa undani zaidi

EPUKA KUPAKUA APPS HIZI KUTOKA MASOKO YASIYO RASMI!

 • Perfect Cleaner
 • Demo
 • WiFi Enhancer
 • Snake
 • gla.pev.zvh
 • Html5 Games
 • Demm
 • memory booster
 • แข่งรถสุดโหด
 • StopWatch
 • Clear
 • ballSmove_004
 • Flashlight Free
 • memory booste
 • Touch Beauty
 • Demoad
 • Small Blue Point
 • Battery Monitor
 • 清理大师
 • UC Mini
 • Shadow Crush
 • Sex Photo
 • 小白点
 • tub.ajy.ics
 • Hip Good
 • Memory Booster
 • phone booster
 • SettingService
 • Wifi Master
 • Fruit Slots
 • System Booster
 • Dircet Browser
 • FUNNY DROPS
 • Puzzle Bubble-Pet Paradise
 • GPS
 • Light Browser
 • Clean Master
 • YouTube Downloader
 • KXService
 • Best Wallpapers
 • Smart Touch
 • Light Advanced
 • SmartFolder
 • youtubeplayer
 • Beautiful Alarm
 • PronClub
 • Detecting instrument
 • Calculator
 • GPS Speed
 • Fast Cleaner
 • Blue Point
 • CakeSweety
 • Pedometer
 • Compass Lite
 • Fingerprint unlock
 • PornClub
 • com.browser.provider
 • Assistive Touch
 • Sex Cademy
 • OneKeyLock
 • Wifi Speed Pro
 • Minibooster
 • com.so.itouch
 • com.fabullacop.loudcallernameringtone
 • Kiss Browser
 • Weather
 • Chrono Marker
 • Slots Mania
 • Multifunction Flashlight
 • So Hot
 • Google
 • HotH5Games
 • Swamm Browser
 • Billiards
 • TcashDemo
 • Sexy hot wallpaper
 • Wifi Accelerate
 • Simple Calculator
 • Daily Racing
 • Talking Tom 3
 • com.example.ddeo
 • Test
 • Hot Photo
 • QPlay
 • Virtual
 • Music Cloud
SOMA PIA:  AzamTV App yapakuliwa zaidi ya mara milioni moja

Kama wewe pia ni mtumiaji wa app kutoka katika soko lisilo rasmi basi unaweza kuangalia katika ukurasa huu – https://gooligan.checkpoint.com/ kwa kuwasilisha anuani yako ya barua pepe na wao wataangalia kama akaunti yako imeshambuliwa.

 

Kama kweli umeshambuliwa unatakiwa kwanza kubadilisha neno la siri la akaunti yako ya Gmail mara moja na pia utahitaji kuipeleka simu kwa mafundi wanaotambulika na wazoefu ili waweze ku’flash simu hiyo (au ku- install upya OS katika simu yako).

SOMA PIA:  'Wasiojulikana' waiba simu za iPhone X zenye thamani ya 826 milioni

Endelea kushiriki pamoja na sisi katika maada mbalimbali za teknolojia katika lugha yako ya kiswahili.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com