Siri: Programu ya Apple yaita ambyulensi kumsaidia mtoto

0
Sambaza

Mwanamke mmoja kutoka Cairns Australia, alitumia programu ya Apple “Siri” kupigia simu ambyulensi (gari ya kubebea wagonjwa) kwa mtoto wake wa mwaka mmoja alipokuwa na tatizo la kupumua.

Siri ni nini? Siri ni programu tumishi inayomilikiwa na Apple yenye uwezo wa kujibu chochote utakachouliza na hata kusaidia kutoa huduma ya dharura mara tu inapoamuliwa.

Mama akiwa na mtoto wake

Mama akiwa na mtoto wake

Bi. Stacey Gleeseon alichukua simu yake na kukimbia hadi chumba cha mtoto ili kumsaidia lakini akaiangusha simu hiyo alipowasha taa. Alipiga kelele akiitaka simu hiyo kuamsha programu ya Siri na kuiambia programu hiyo kuita huduma ya dharura (emergence service) huku akianza kumfufua mtoto huyo.

Bi. Gleeson aliamini huduma hiyo inaweza kuokoa maisha ya mwanawe. Aliamrisha app ya SIRI kuita ambyulensi na aliweza kuzungumza na huduma hiyo ya dharura huku akijaribu kumwamsha mwanae mwenye umri wa mwaka mmoja aliyekuwa amezimia.

Application ya Siri

Application ya Siri

Application hiyo (Siri) haipo kwenye haipo kwenye aina zote za iPhone hivyo basi ili kuweza kujua kama iPhone yako ina Siri nenda kenye Settings>General>Siri halafu iweke “On”.

Application hiyo ambayo inaaminika kujizolea umaarufu kutokana na kuokoa maisha ya mtoto mdogo ingawa mmliki wa simu hiyo alikuwa mbali nayo. Mtoto Giana alianza kupumua tena wakati ambyulensi hiyo ilipowasili. Mama Giana anatumia Iphone 6S na kuahidi kuwa kamwe hatoizima application ya Siri.

SOMA PIA:  VKWorld Z3310: Kopi ya simu ya Nokia 3310 (2017) yatoka kwa bei nafuu

Je, unadhani application hii itakuwa tunu kwa Tanzania katika kuokoa maisha ya mgonjwa? Tuandikie maoni yako hapo chini.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com