Sirius A: Kompyuta ya Windows 10 inayotosha mfukoni mwako

Sirius A: Kompyuta ya Windows 10 inayotosha mfukoni mwako

0
Sambaza

Kutana na Sirius A, hii ni kompyuta ndogo isiyokuwa na ata feni ndani yake. Sirius A imetengenezwa na kampuni ndogo tuu inayojulikana kama Ockel Computers iliyokuja na wazo la bidhaa yake kupitia huduma ya kutafuta mitaji ya IndieGogo.

http://vanbeverlawfirm.com/tag/faq/ Ingawa ni ndogo, ata kuzidi baadhi ya tableti bado Sirius A ina uwezo wa kuwa kompyuta kamili pale inapounganishiwa na keyboard, mouse/kipanya na TV/Monitor.

see kompyuta ndogo sirius a

Sirius A ina ukubwa wa inchi 6 tu na inakuja na kilo (display) ya mguso (touchscreen). Display yake ni ya kiwango cha HD cha 1080p.

Pia inakuja na kamera ya mbele (selfi) pamoja na teknolojia ya kutambua alama za vidole (fingerprint sensor).

INAYOHUSIANA  NMB, Halotel kutoa huduma za TEHAMA bure mashuleni

http://dazzlingdwelling.com/wp-content/plugins/page-google-maps/css/default.css Betri la mAh 3,000 – Ocket Computers wanasema utaweza kutumia kompyuta yako popote ulipo kwa hadi massa 3.

kompyuta sirius

Bila kuiunganisha na vifaa vingine bado unaweza kuitumia kama kawaida.

Je ina tofauti gani na tableti za kawaida?

kompyuta serius a

Ikiunganishwa na vifaa kama vile monitor/tv, keyboard na kipanya..utaweza kuitumia kama kompyuta kamili.

Kuonesha uwezo wake mkubwa kama kompyuta na si kuwa sehemu moja na tableti zinazotumia Windows Sirius A inakuja na ports mbalimbali na sifa zingine za kompyuta;

  • Maeneo mawili ya USB 3.0 pamoja na moja ya USB Type C
  • Eneo la waya HDMI, DisplayPort na intaneti ya waya – Ethernet
  • Pia kuna sehemu ya Umeme wa V 12.
  • Pia ina WiFi na Bluetooth 4.2
INAYOHUSIANA  Biashara ya kwanza kufanyika mtandaoni

Kuna matoleo mawili, kuna toleo la Sirius A linalotumia Windows 10 Home 64bit, hili linakuja na prosesa ya Intel Atom na RAM ya GB 4 na diski ya SSD ya GB 64. Pia kuna toleo la Sirius Pro, hili linakuja na RAM ya GB 8 na diski ya SSD ya GB 128.

Kompyuta ndogo sirius A

Sifa kwa undani za kompyuta ya Serius A na Serius A Pro

Bei zake zitakuwa kati ya Tsh 1,200,000 hadI Tsh 1,500,000. Na kupitia mtandao wao watatuma bidhaa hiyo kwa mnunuaji yoyote katika nchi mbalimbali.

Fahamu zaidi: IndieGogo | Ockel

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.