Skype Kutengenezwa Upya Kuwa Kama Snapchat Kwa Microsoft!

0
Sambaza

Skype ni mtandao wa maswala ya kupiga na kupokea simu kwa kutumia huduma ya mtandao. Pia katika mtandao huo unaweza ukafanya mambo mengine kama vile kutuma na kupokea ujumbe wa maandishi.

Kwa upande mwingine mtandao wa Snapchat umekua na mafanikio makubwa na umaarufu wa hali ya juu na jambi hili limeifanya mitandao mingine kuumiza kichwa na katika kuhakikisha wanakuja na njia kabambe za kuushinda mtandao huu.

Skype ni mtandao kabambe lakini kwa siku hizi upo kama unapotelea hivi? hii kampuni ya Microsoft imeliona na ndio maaana wako tayari kufanya maboresho makubwa (kutengeneza upya) mtandao huo.. Na kwa sasa ni kwamba mtandao unaweza ukatengenezwa kwa kufuata nyayo za Snapchat.

Muonekano Mpya Wa Skype

Maboresho makubwa mapya ambayo yanatolewa macho yanajulikana kama ‘Highlight’ na ‘Capture’ .

SOMA PIA:  Jinsi ya kuzuia iOS 11 kumaliza chaji ya simu yako ndani muda mchache

Capture itamuwezesha mtumiaji kupiga picha na video ambazo wanaweza kuzi’share na marafiki (contact) ndani ya Snapchat.

Highlight ni pale picha na video zitakuwa zinaonekana katika ukurasa wa mtu husika. Hii itawezesha watu kujua ni kitu gani mtu anafanya kwa siku hiyo …. Kidogo inafanana kama Stories.

Microsoft kwa upande wao hawakukataa kama wameigilizia jambo hili kutoka kwa mtandao wa kijamii maarufu wa Snapchat

Muonekano Wa Zamani Wa Skype

Snapchat ilianzishwa mwaka 2011 na ukawa na umaarufu mkubwa ndani ya kipindi cha muda mdogo sana.

SOMA PIA:  Sio ndani dakika 7 tu! Unaweza kufuta ujumbe hata baada ya siku 7 katika WhatsApp #Maujanja

Ningependa kusikia kutoka kwako. Niambie hili unalichukuliaje? je Skype itarudi katika hadhi yake? Niandikie hapo chini sehemu ya comment

Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com