Skype – Wakuwezesha Kuchati na Kuzungumza na Watu Mbalimbali KTK Lugha Zao Bila Wewe Kuzifahamu!

0
Sambaza

Programu ya kuchati na kupiga simu ya Skype imekuja na uwezo mpya kuanzia sasa utakaopatikana kwa watumiaji wote duniani kote, uwezo wa kuchati au kuongea katika lugha tofauti na mtu mwingine na meseji zenu kuweza kutafsiriwa muda huo huo na hivyo kuelewana.

Kampuni ya Skype inayomilikiwa na kampuni kubwa ya Microsoft ilishatangaza kuwa inatengeneza teknolojia hiyo tokea mwaka jana, na sasa watu wote wanaotumia programu endeshaji wa Windows wataanza kutumia teknolojia hiyo.

Mazungumzo katika simu ya video (Video call) yakitafsiriwa eneo la chini
Mazungumzo katika simu ya video (Video call) yakitafsiriwa eneo la chini
SOMA PIA:  Miaka 30 ya mafaili ya mtindo wa GIF. - Fahamu historia yake!

Inafanyaje Kazi?

  • Fikiria kuna mtu mmoja anajua kiingereza tuu wakati mtu mwingine anazungumza kihispania tuu
  • Mmoja akiandika meseji/ujumbe na kumtumia mwingine ujumbe huo utapokelewa ukiwa katika lugha atakayoichagua yeye ili kumuwezesha msomaji kuweza kuuelewa katika lugha yake.
  • Naye akijibu katika lugha yake msomaji wa upande wa pili ataupokea katika lugha yake.
  • Kwa kupiga simu utafsiri huo utafanyika na kuweza kusomeka kwa maandishi
  • Katika kuchati mpokeaji atapokea meseji katika lugha zote mbili, ya mtumaji ya yeye msomaji.
Tafsiri ya Mazungumzo Yaliyo ktk Chati
Tafsiri ya Mazungumzo Yaliyo ktk Chati
SOMA PIA:  Kwanini blog nyingi za kitanzania hufa?

Kwa sasa uwezo huo wa utafsiri lugha kwa watu wanaopigiana simu unafanya kazi kwa lugha ya kiingereza, kihispania, kiitaliano na kichina (mandarini), wamesema wanategemea kuweza kuongeza lugha zingine taratibu.

Ila kwa wanaochati kwa kutumia kuandikiana ujumbe teknolojia hii inafanya kazi kwa zaidi ya lugha 50, kwa sasa kiswahili si moja ya lugha hizo, ila tutegemee itakuja hapo mbeleni.

Arabic English Hungarian Maltese Slovak Yucatec Maya
Bosnian (Latin) Estonian Indonesian Norwegian Slovenian
Bulgarian Finnish Italian Persian Spanish
Catalan French Japanese Polish Swedish
Chinese Simplified German Klingon Portuguese Thai
Chinese Traditional Greek Klingon (plqaD) Queretaro Otomi Turkish
Croatian Haitian Creole Korean Romanian Ukrainian
Czech Hebrew Latvian Russian Urdu
Danish Hindi Lithuanian Serbian (Cyrillic) Vietnamese
Dutch Hmong Daw Malay Serbian (Latin) Welsh
SOMA PIA:  Milioni 7 wakosa huduma za simu baada ya shambulizi la kimtandao Venezuela

Kuwezesha teknolojia hii katika Skype yako itabidi ushushe na kupakua programu ya Skype Translator katika kompyuta yako yenye programu ya Skype.

Shusha Skype (Bofya) | Skype Translator (Bofya)

Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia katika lugha ya kiswahili, TeknoKona!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com