Google wazidi kuwekeza katika teknolojia za kiakili – ‘artificial intelligence’ katika kufanya mfumo wa barua pepe wake wa Gmail kuwa bora zaidi hasa kwa watumiaji wa app ya Gmail katika simu za Android na iOS.
Smart Reply: Teknolojia hii itaanzia kwa watumiaji wa app ya Gmail kwenye iOS na Android. Lengo kuu ni kutumika kwenye simu.
Kutakua na majibu yatakayokuwa yanapendekezwa na hivyo kukupunguzia ulazima wa kuandika, pia kama utaitaji kuboresha jibu ilo basi utaweza kuboresha kabla ya kubofya ‘Send/Tuma’.
“Zaidi ya nusu ya barua pepe zote zinazosomwa huwa zinasomwa kwa kutumia simu”
Kwa kila utakavyokuwa unajibu barua pepe zako basi mfumo huo utakuwa unazidi kujifunza jinsi majibu hayo unavyoyaandika na utaweza kuona mapendekezo ya majibu yenye ukaribia na vile ambavyo huwa unajibu.
Teknolojia hiyo itakuja kupatikana katika lugha ya kiingereza na Google hawajatoa taarifa kama itasambaa kwenye lugha zingine pia. Je wewe unasoma na kujibu barua pepe kwenye kompyuta au simu zaidi?
One Comment