Smarttress – Mpenzi akikusaliti kitandani kwenu utapata taarifa mara moja

0
Sambaza

Utafiti mmoja umewaweka wanaume na wanawake wa nchini Uhispania kwenye orodha ya watu wanaoongoza kwa kutokuwa waaminifu kwa wenzi wao – na sasa kampuni moja nchini humo imekuja na njia ya kutatua tatizo hilo. Kitanda janja kitakachotuma taarifa pale kinapotumiwa.

smarttress kitanda janja

App ya Smarttress ikionesha taarifa

Godoro janja hili lililopewa jina la Smarttress – muunganisho wa Smart Mattress (Godoro janja), limetengenezwa na kampuni moja ya magodoro inayokwenda kwa jina la Durmet ya huko nchini Uhispania. Godoro hilo lina teknolojia za sensor ndani yake kwa ajili ya kutambua mabadiliko mbalimbali mfano kama sehemu flani imekaliwa na ni kwa uzito gani n.k.
smarttress godorosmarttress
Godoro hili lina sensors 24 (ultrasonic sensors), kupitia sensors hizi godoro hilo litaweza kutuma ujumbe(alerts) kwenda kwa watumiaji wa kitanda hicho kupitia app yake ambayo inabidi watumiaji kitanda wawe nayo kwenye simu zao.
App hiyo itapata taarifa zote kuhusu utumiaji wa Godoro hilo, eneo gani limetumika zaidi, na kama ni watu walikuwa kwenye kitanda hicho walikuwa eneo gani hasa na kwa kasi gani walikuwa wanahama hama kitandani…
IoT – Internet of Things...ni utumiaji wa teknolojia za kiwamasiliano kama vile intaneti katika utengenezaji wa bidhaa ambazo kabla isingekuwa rahisi kufikiria uboreshwaji ufanyaji kazi wa vifaa hivyo kupitia teknolojia kama intaneti. Kwa sasa eneo la teknolojia la IoT linakua kwa kasi sana. Kuna vitu vingi kama vile mafriji, taa, n.k vinaunganishwa katika mfumo wa apps na huduma ya intaneti.

Je una mtazamo gani juu ya teknolojia hii?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Chip mpya ya Qualcomm: Simu za bei nafuu (Featured phones) kuja na uwezo wa 4G LTE
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com