Snapchat Kuleta ‘GeoStickers’ Katika App Yao!

0
Sambaza

Kama ni mtumiaji mzuri wa Snapchat, utakuwa unajua kwamba kuna kitu kinaitwa ‘GeoFilters’ yaani ni zile ‘Filter’ zinazotokea ukiwa katika eneo Fulani mfano Dar es salaam (bongo land), Sinza n.k.


Hivi sasa wameona haitoshi wameamua kuja na filter maalumu kwa ajili ya stika maarufu kama ‘GeoStickers‘. Yaani hapa stika ndio zitakua zinatambulisha eneo. Kwa mfano hebu fikiria labda ukiwa katika maeneo ya posta (Dar es salaam) unaweza ukatumia stika la lile sanamu la askari? – fikiria tuu! – itakua ni poa sio?.

SOMA PIA:  TTCL waachana rasmi na teknolojia ya CDMA, sasa ni 3G na 4G tuu


Hiyo ndio dhima kubwa ya ‘Geostickers’, japokuwa mpaka sasa bado maboresho haya yanapatikana katika baadhi ya miji maarufu sana duniani kama vile Los Angeles, San Francisco, New York City, Washington DC, Honolulu, Paris, London, São Paulo, Sydney na Riyadh.
Kama ‘Filter’ zingine zilivyoenea kwa haraka katika nchi na miji mingine duniani, na hizi wembe ni ule ule. Tukae mkao wa kula katika nchi na miji yetu kuweza kupata uwezo huu.

https-%2F%2Fblueprint-api-production.s3.amazonaws.com%2Fuploads%2Fcard%2Fimage%2F164558%2F692399bfd66d4b45bfc0564d8144e88f
Japokua kwa sasa zinapatikana katika miji michache ili kuzitumia katika miji hiyo inabidi katika settings za simu mtu awe amewasha eneo (Location) ndio ataweza kutumia.

snapchat-launches-sponsored-geofilters-stickers-representative-of-users-location-users-can_1
Hizi unaweza pia ukazituma katika meseji au ukaziweka sambamba na snap yako na ukatuma katika stori zako.

IMG_0121
Toleo hili limetolewa na Snapchat hapa

article-2693196-1FAA237B00000578-154_634x368
Tukae mikao ya kula ili hii itufikie katika miji yetu. Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment hii umeipokea vipi?

Tembelea TeknoKona kila siku ili kuwa karibu na habari na maujanja mbali mbali yanayohusu teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com