Snapchat: Ndani ya Muonekano mpya! #Masasisho - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Snapchat: Ndani ya Muonekano mpya! #Masasisho

0
Sambaza

Snapchat imepata mabadiliko ya muonekano katika update yake ya hivi karibuni, mabadiliko hayo yanazidi kurahisisha jinsi ya kutumia app hiyo.

Pamoja na mabadiliko ya kimuonekano app hii imeongeza uwezo wa watumiaji kuweza kujiandikisha katika kurasa za habari wanazozipenda.

Snapchat app ambayo imekuja kwa kasi na ndani ya muda mfupi imeweza kupata umaarufu mkubwa kwa watumiaji wengi, inayaleta mabadiliko haya ya kimuonekano na kimuundo ili iweze kuwavutia watumiaji kuendelea kuwa hai huku pia ikiwavutia watumiaji wa mara ya kwanza.

 muonekano

Ukurasa wa discover ulivyo kuwa unaonekana siku zamani

Mabadiliko ya muonekano yaliyoletwa na Snapchat katika update yao hivi karibuni ni;

INAYOHUSIANA  Apple wafanya iwe vigumu zaidi ku'hack iPhone kwa Kuzima Uwezo wa USB

Kuanzia sasa kurasa kuu zote zitakuwa na vitufe vitatu ambavyo vinawakilisha kurasa kuu tatu za Snapchat mtumiaji ataweza ku gusa ili kwenda katika ukurasa husika, Ukiwa katika ukurasa wa kuchat kwa mfano unaweza kugusa na kwenda ukurasa wa kamera ama kugusa kwenda ukurasa wa stories ambao ndio unakuwa na stories za marafiki zako.

  • buy avodart 0.5mg Sasa unaweza kujua kilichomo ndani ya video ama picha ya mtu kabla hujafungua

Snapchat wameleta uwezo kwa mtumiaji kujua nini kimo katika video ama picha za mtu kabla ya kuifungua video ama picha hiyo, hii itawasaidia watumiaji kuepuka aibu kwa kufungua vitu ambavyo hawakujua kama kwa namna moja ama nyingine vingekuwa vya kuaibisha.

Muonekano

Jinsi stories zinavyoonekana baada ya mabadiliko

Kwa sasa muonekano mpya unaathiri zaidi Discover ambayo kwa namna fulani imefanywa iweni rahisi kwako kuangalia na kujisomea habari tofauti tofauti.

muonekano

Jinsi ukurasa wa discover unavyoonekana sasa

  • Na pia kwa sasa utaweza kujiunga na chaneli mbali mbali ili usikose habari muhimu.
INAYOHUSIANA  WhatsApp inaweza kuchezewa

Huduma hii mpya itawasaidia watumiaji saana hasa ili wasikose habari ambazo wanazipenda, kwa kujiunga na chaneli fulani ambayo inatoa habari fulani yaani kuji subscribe basi chaneli hiyo itakuwa wakati wote inatokea katika ukurasa wako wa discover.

 

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.