Snapchat Waanzisha Ma’Group’ Na Vipengele Vingine, Sasa Chat Mpaka Na Watu 16!

0
Sambaza

Baada ya mitandao mingi kuwa na makundi ya aina mbali mbali ambapo watu wanaweza wakaongea mambo yao wakiwa zaidi ya wawili na kuendelea mtandao wa Snapchat nao umeona ni vyema kuliwezesha hilo.

Kipengele cha ‘Group’ katika mtandao huu kimeongezwa ambapo hapo utakuwa na uwezo wa kuongea mpaka na watu 16 katika kundi moja.

Hii inasaidia sana kwani mtu badala ya kutuma picha moja kwa kila mtu, itakuwa ni rahisi kabisa ukiwa unatuma picha moja katika kundi ambayo itamfikia kila mtu.

Snapchat

Snapchat

Nna imani faida ya makundi unaijua kwa sana tuu maana yamekuwa yakifanikisha mengi. Kipengele hiki kimetoka wakati mzuri kabisa kwani huu ni wakati wa sikukuu za kumalizia mwaka.

SOMA PIA:  AppStore: Apple yaondoa VPN kwa simu za iPhone nchini China

Jinsi Ya Kutengeneza ‘Group’.

Ni rahisi sana kwani itakubidi urekodi video au upige picha kama kawaida na kisha ubonyeze kile kimshale cha bluu upande wa chini wa kulia wa video/picha yako.

Baada ya hapo itakubidi uchague watu (marafiki) zake ambao unataka uwatumie hiyo video/picha katika group. Ukishamaliza tuu kuwachagua, upande wa juu kabisa bonyeza alama ya ‘New Group’ (vikatuni vitatu).

Jinsi Ya Kutengeneza Group

Jinsi Ya Kutengeneza Group

‘Group’ hilo jipya litahifadhiwa na kuwa linapatikana chini ya marafiki zako wengine. Na kama ilivyo kawaida hata snap ambazo zinatumwa katika ma’Group’ ni kwamba zitafutika kila baada ya masaa 24 kila zinapotumwa.

SOMA PIA:  Jinsi Ya Ku'Log Out' Instagram Kwa Kutumia Kifaa Kingine!

Mtu kama ukiingia katika ‘Group’ na wenzako watapata taarifa na kujua kama wewe upo ndani ya group hilo kwa wakati huo.

Mambo mengine ambayo yanaweza kuonekana/kujulikana ni pamoja na itaweza fahamika nani kasoma au kasevu snap. Vilevile katika ‘settings’ ya kundi mtu ana uwezo wa kubadilisha jina la kundi na kuhariri ‘notification’.

Jinsi Ya Kuchat Katika Group

Kingine cha muhimu ni kwamba katika ma’group’ ni kwamba hakutakuwa na uwezo wa kupiga simu au hata kuwasiliana kwa kutimia video.

Ukiachana na hii ishu ya Group vile vile Snapchat wameongeza vipengele vingine viwili kikiwemo cha mkasi na cha brashi la rangi (Scissors, Paint Brush).

SOMA PIA:  Ndege isiyotumia mafuta yatua Misri

Hiki cha mkasi kitakuwezesha wewe mtumiaji kuweza kukata eneo flani katika snap yako na kutumia kama stika.

Na kipengela cha mwisho ni hichi cha brashi la rangi ambacho kitamuwezesha mtu kuwewa kupata rangi snap zake katika eneo la ‘memories’


Hapa huna budi kusasisha kifaa chako kufika katika toleo jipya zaidi ili kuweza kufurahia vipengele hivi.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment. TeknoKona daima tupo nawe katika teknolojia!.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com