Snapchat Waja Na Teknolojia Ya Miwani Inayoitwa ‘Spectacles’!

0
Sambaza

Ni wazi kuwa teknolojia ya miwani kama kifaa cha kielektroniki kwa sasa zimejaa, kumbuka hata Google wanayo kama hii inayofahamika kama Google Glass.

Ukiachana na Google, mtandao wa kijamii ambao ulijipatia umaarufu wake kwa video na meseji zinazopotea yaani Snapchat nao wamekuja na teknolojia ya miwani.

Spectacles ni miwani janja ambayo inatumika katika kurekodi video za Snapchat bila ya mtumiaji kutumia simu katika kurekodi video hizo (miwani na simu vitakua vimeunganishwa).

Spectacles

Spectacles

CEO wa Snapchat ndiye alietangaza ishu hii na fununu zingine zilisambaa kwamba kampuni hilo linataka kubadilisha sura yake kwa ujumla na hii inapelekea mpaka kubadilisha jina lake na kuwa Snap Inc.

SOMA PIA:  Matumizi ya simu janja pamoja na 'Drones' katika kupambana na Malaria

Tujie Vitu Ambavyo Spectacles Inaweza Ikafanya.

– Kazi yake kubwa ni kurekodi video fupi fupi za sekunde 10 na kamera (yenye nyuzi 115) iliyoambatanishwa katika katika miwani hiyo.

– Aina za video zinazorekodiwa na Spectacles ni zile zenye mfumo wa umbo la duara. Na hii ni kwa sababu inawasilisha video hizo kwa namna jicho la mwanadamu linavyoona.

– Jinsi ya kurekodi video itakubidi ubonyeze kitufe juu ya miwani hiyo. Ili kumaliza kurekodi itabidi ubonyeze tena kitufe hicho au usubiri mpaka sekunde 10 zipite.

SOMA PIA:  Apple kuja na simu rununu zenye uwezo wa kukunja na kukunjua

– Miwani hii itakuwa inauzwa dola 130 za kimarekani kama zikiingia sokoni.

Bado haijajulikana tarehe ya miwani hii kuingia sokoni rasmi. Haya ndio mambo TeknoKona inayojua mpaka sasa, yakitokea mengine tutakujulisha zaidi.

Spectacles

Spectacles

Angalia Video Hii Kuangalia Video Za Spectacle Zinavyokua.

Niambie hii umeipokeaje? Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Tembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com