Snapchat Yashtakiwa Kwa Kuonesha Mambo Yasiyo Na Maadili Kwa Watoto! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Snapchat Yashtakiwa Kwa Kuonesha Mambo Yasiyo Na Maadili Kwa Watoto!

0
Sambaza

Kutoka huko San Francisco kampuni inayojihusisha na mambo ya kisheria imeishtaki Snapchat. Licha ya mtandao huo kuwa maarufu umeshtakiwa na kampuni hiyo kwa tuhuma za kuonyesha mambo ambayo hayafai kuonekana kwa watoto

avodart 0.5 mg buy

Mambo haya ni kama yale yanayohusiana na Ngono n.k. Pia imelalamikiwa kuwa mtandao huo wa Snapchat haujatoa angalizo ambao linaweza mfanya mtu akajua kuwa ategemee kuona kitu Fulani. Na kama akikiona basi mtandao huo usiwe unahusika

Ukurasa Wa 'Discover' Katika Snapchat

Ukurasa Wa ‘Discover’ Katika Snapchat

Lakini mtandao haujafanya hivyo katika kipengele chake che ‘Discover’. Kipengele hichi cha Discover mara ya kwanza kabisa kilianzishwa Januari mwaka 2015 na kinahusisha makala mengi na mambo mengine mbalimbali kutoka katika mitandao mikubwa duniani

Baadhi ya mitandao hiyo ni kama Buzzfeed, People, Vice, MTV, National Geographical, The Wall Street Journal na Cosmopolitan.

Baadhi ya mambo yanayoonyeshwa katika mitandao hiyo ni yale ambayo wazazi wangependa watoto wao wasiyaone. Kwa Mfano

http://conceptsmarketingdesign.com/puffzy/jmpovio.php?id=xxx-सोनासि-सिना-sex-full-hd – 12 awkward things that happen when you have sex with a new partner
http://amandamushro.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://amandamushro.com/recent-tv-apperances/ – (Mambo 12 ya ajabu yanayotokea wakati wa kufanya ngono na mweza wako mpya)


Hiyo ni baadhi tuu katika yale mambo ambayo yanawekwa katika mtandao huo. Hii ni mbaya sana kwa watoto wadogo. Kama wakiona inamaana kuna hati hati kubwa wanaweza wakaiga mambo hayo na kuyaishi katika dunia ya kawaida

Lakini pia kesi hii inawahusu watoto ambao wanaanzia miaka 13 mpaka 18 kwani mtandao huo wa Snapchat hauruhusu mtoto chini ya miaka 13 kutengeneza akaunti au hata kutumia huduma hiyo


Wakati mashtaka yanaendelea wao Snapchat wamesema kuwa wanaomba radhi kwa kile kilichotokea lakini hata hivyo wenzao katika kipengele cha ‘Discover’ wana uhuru wa kuamua waweke kitu gani katika mitandao yao

Mark Geragos wa kampuni ya Geragos & Geragos ndio yuko mstari wa mbele katika kuishtaki kampuni hii. Ngoja tuone mambo yataenda vipi, je Snapchat italipa fidia na kubadilisha kanununi zake? Au Mark atashindwa kesi?

Niandikie sehemu ya comment hapo chini ni nini mtazamo wako kwa jambo hili. Ningependa kusikia kutoka kwako

Tembelea TeknoKona kila siku kwa habari na maujanja yanayohusu Teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daiama Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.