Snowden anatengeneza vifuko vya kiusalama kwa ajili ya iPhone 6

0
Sambaza

Yule aliyeyaweka wazi yale mabaya yanayofanywa na shirika la kijasusi la Marekani kuhusu kufuatilia watu kupitia simu na vifaa vingine sasa kutengeneza vifuko vya kuhifadhia simu ya iPhone 6 na kuzuia kufuatiliwa.

Soma Pia – Snowden ajiunga Twitter

Kwa ushirikano na Andrew “Bunnie” Huang, Snowden anatengeneza vifuko kwa ajili ya iPhone 6 ambavyo vitakuwa na uwezo wa kuhisi kama simu yako inatuma taarifa(data) hata kama ikiwa imezimwa huku ikitakiwa kutofanya hivyo.

Kifuko cha simu ya iPhone 6 chenye uwezo wa kuzuia simu yako kufuatiliwa

Kifuko cha simu ya iPhone 6 chenye uwezo wa kuzuia simu yako kufuatiliwa.

Lengo ni kuwasaidia waandishi wa habari, watu wanaoshughulikia haki za binadamu kutofuatiliwa na serikali au mamlaka nyingine wakiwa wanafanya kazi zao na kuibua maovu mbalimbali kutokana uchunguzi wao.

Kifuko hicho kitakuwa na nyanya ambazo zitaweza kupata taarifa kutoka wenye antena ya simu kupitia sehemu ya kuweka sim card kwa ajili ya ku-monitor usafirishwaji wa masafa(signals) pia kuwa na alarm itakayomtaarifu mtumiaji hali ya simu.

SOMA PIA:  Fikiria Simu Bila Ya Betri, Teknolojia Hii Ipo Katika Hatua Zake Za Kwanza!

iPhone 6's hat

Vifuko hivi bado vipo katika hatua ya awali ya utenezwaji lakini tayari Snowden na mwenzake wameshachapisha andiko linaloelezea jinsi vifuko hivyo vitakavyokuwa.

Kifuko hiki kinaweza kisiwe na wapenzi wengi hasa kwa wale vibaraka wanaotegemea kula yao kutokana na kufuatilia ya watu na kupeleka taarifa zao kwa wanaozihitaji ila vitakuwa na faida kwa waandishi wa habari ambao wao daima wanafuatiliwa kwa karibu sana kutokana na asili ya kazi zao. TeknoKona tutaendelea kufuatilia kwa karibu vifuko hivi na kuwajuza.

SOMA PIA:  Google Assistant sasa inaweza kujua jina la wimbo unaoimba kwenye simu janja #Masasisho

Soma Pia – Snowden ajiunga Twitter

Vyanzo: TnW, MacRumors

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com