Solarin; Ifahamu Simu ya Tsh Milioni 36.5 (Dola 16,600)

Solarin; Ifahamu Simu ya Tsh Milioni 36.5 (Dola 16,600)

0
Sambaza

Unaweza ukafikiri ni utani, ila ukweli ni kwamba simu hii ipo na kama unaiitaji basi itakubidi kutoa takribani Tsh Milioni 36.5 (Ksh Milioni 1.6). Solarin ni simu kwa wanaopenda ulinzi na usalama wa data zao.

Pia kumbuka bei hii ni kabla ya kodi, inaonekana baada ya kodi basi bei yake itakuwa juu ya ata Tsh milioni 40 za Kitanzania (Zaidi ya dola 20,000 za kimarekani).

Simu ya Solarin; Inakuja katika rangi mbili

http://reenajbhambra.com/?feed=rss2 Simu ya Solarin; Inakuja katika rangi mbili

 

simu ya Sirin Labs Solarin

enter Solarin inatengenezwa na kampuni ya kiisraeli

Inatengenezwa na nani?

Simu hii ya inchi 5.5 inayotumia Android inatengenezwa na kampuni mpya tuu ifahamikayo kwa jina la Sirin Labs. Kampuni hii makao makuu yake ni nchini Israeli

Ni kwa ajili ya kina nani?

Simu inauzwa kama ni chaguo kwa watu wanaotaka usalama wa kiwango cha juu wa data za simu zao. Ingawa ni ukweli usiopingika ya kwamba Android yenyewe kama yenyewe pia inakuja na mifumo ya kiusalama,…na bado pia unaweza pata usalama zaidi kupitia simu zingine kama vile BlackBerry Priv na pia simu za Samsung zinazokuja na mfumo wa usalama unaofahamika kama Knox zote kwa bei nafaa ukilinganisha na bei ya Solarin.

INAYOHUSIANA  Uber waanza na India kutoa toleo dogo kabisa la programu tumishi

Kwa nyuma eneo la kamera, kuna switchi ambayo ikiwashwa basi uwezo wote wa kisimu janja (smartphone) huzimwa…na hivyo mtumiaji ataweza kutuma sms na kupiga simu tuu. Hali hii huifanya simu hiyo kuwa ata vigumu zaidi kudukuliwa.

Simu Solarin

Solarin simu

Simu ya Solarin – Hapa ni muonekano wake switchi ya kuzimu sifa za simu janja ikiwashwa

Ilivyotambulishwa rasmi Jumanne wiki iliyopita mastaa wa filamu kama vile Leonardo DiCaprio na Tom Hardy walishiriki – hili linaonesha ni jinsi gani simu hii inawalenga hasa watu kama vile viongozi wa kibiashara, mastaa, matajiri n.k na si kwa ajili ya watumiaji wa kawaida ambao kwa bei hii simu hii inaonekana ni kituko kabisa.

INAYOHUSIANA  Utoaji wa talaka kwa njia ya simu wakemewa

Sifa za Kiundani za Simu ya Solarin

Kampuni ya kiisraeli ya Sirin Labs inayotengeneza simu hiyo imesema`simu hiyo inakuja na kasi ya intaneti ya hadi mara 10 ukilinganisha na simu nyingine za 4G zilizopo kwa sasa.

Ina http://pottervalley.org/?s= mifumo mingi zaidi ya 4G (bands za 4G) kuliko simu nyingine iliyopo sokoni. Hii ikimaanisha utaweza kutumia simu hiyo kwenye mitandao tofauti tofauti zaidi ya 4G.

  • Teknolojia yake ya WiFi inakubali intaneti ya kasi ya hadi mara 10 ukilinganisha na kasi za intaneti zinazopatikana kwa sasa
  • Spika zinazokuja katika simu hiyo ni za ubora wa hali ya juu. Ina spika 3, 2
  • Kioo (display) ni cha inchi 5.5
  • Kamera ya megapixel 23.8 ikija na teknolojia za ‘autofocus’ pamoja na uwepo wa flash kwa kamera ya selfi – yenye megapixel 8
  • Prosesa ya Snapdragon 810
  • Uzito wa gramu 250
  • Betri mAh 4,000
  • Kiwango cha RAM cha GB 4 na diski uhifadhi (storage) wa GB 128
INAYOHUSIANA  Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand

Una maoni gani kuhusu simu hii na bei yake? Je unadhani unakitu cha kuficha kwenye simu yako ambacho uko tayari kutumia zaidi ya milioni 30 kwa ajili ya kukilinda?

Soma Pia –

Vyanzo: theVerge, CNN na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.