SolidEnergy: Teknolojia mpya kufanya betri zidumu mara mbili zaidi

0
Sambaza

Wanafunzi na watafiti wa chuo kikuu cha MIT (Massachusetts Institute of Technology) cha nchini Marekani wameweza kugundua teknolojia mpya ya kutengeneza betri kwa ajili ya vifaa mbalimbali kama vile kamera na simu itakayohakikisha mabetri yanakuwa madogo na huku ya kiwa na ujazo wa chaji mara mbili zaidi.

solidenergy betri

Mlinganisho wa muonekano wa betri, kulia ni betri kutoka SolidEnergy, betri dogo zaidi lakini ujazo mara mbili ukilinganisha na mengine

Kampuni waliyoitengeneza kutokana na mafanikio hayo, SolidEnergy Systems inategemewa kufanya uzinduzi wa mara ya kwanza kabisa ya mabetri kwa ajili ya kuuzwa ifikapo mwezi Novemba.

SOMA PIA:  Namna ya kuwa WhatsApp Tester (Tumia toleo la beta) #Maujanja

Mabetri yatakayotoka kwa mwanzo yatakuwa kwa ajili ya kutumika kwenye ‘drones’ lakini ni mategemeo muda si mrefu teknolojia hiyo itatumika kwa ajili ya mabetri ya simu janja, kamera na vifaa vingine vidogo vya elektroniki.

Kilichobadilika zaidi ni nini?

Inasemekana wakati mwanafunzi Qichao Hu akiwa anafanya kazi na Profesa wake alifanikiwa kugundua njia ya kutengeneza betri la kisasa kwa kuondoa ‘anode’ ambazo zinasifa za kuchukua nafasi kubwa ya betri na badala yake akatumia mfumo mpya unaotumia malighafi za chuma. Malighafi hizo za chuma zinaweza tunza kiwango kikubwa cha ions (chaji) ukilinganisha na ‘anode’.

SOMA PIA:  Apple Kuja Na Emoji Mpya Katika Vifaa Vya iOs na macOS!

Kupitia kampuni mpya iliyosajiliwa ya SolidEnergy Systems inategemewa teknolojia hiyo itaweza kufanikiwa kuanza kutumika haraka katika aina mbalimbali ya vifaa vya elektroniki vinavyoitaji betri. Hadi sasa kampuni hiyo ishapata wawekezaji waliingiza katika kampuni hiyo zaidi ya dola milioni 12 za Marekani (Zaidi Tsh Bilioni 26).

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com