Kampuni ya SONY imetangaza kuachilia PlayStation VR (Virtual Reality) katika mfululizo wa Michezo ya Bartman :Arkham na Spiderman kwenye toleo lao jipya la Play Station 4.
“Tunajitahidi kufikia kizazi kipya kabisa cha michezo ya TV” aliezelza Peter Phillips, makamu Raisi kampuni ya Marvel, katika maonyesho ya Teknolojia ya E3 mapema wiki hii.
Hili limetazamiwa kama Jibu kwa Microsoft, baada ya kutangaza kuja na toleo jipya kabisa la Xbox litakalokua bora na jembamba zaidi. SONY waliamua kutangaza ujio wa toleo jipya la Play Station 4 na Mfumo wa PS Virtual reality.
Sasa wachezaji wa michezo hii wataweza kufurahia michezo yao katika mashine za kisasa za Virtual Reality, na kupata uzoefu mpya kabisa ambao hawakuwahi kuufikiria.
“Mhusika kama Spiderman, amefanya makubwa kueneza haki katika Jiji la New York.” Alielezea Philips, “Mtazame Peter Paker, wakati wote anahaha kuhakikisha haki inatendeka katika mji uliochafuka kama Gothan. Atafaa sana!”
Hata hivyo, SONY walifanya siri kuachilia baadhi ya tetesi zilizokuwa masikioni mwa watu katika tamasha hilo la E3. Wengi waliokuwa wakisubiri kutangazwa kwa Play Station 4 yenye uwezo wa kipekee zaidi katika tamasha.
SONY pia waliweza majina ya michezo itakayofanya kazi na Play Station VR ikiwa ni pamoja na DAY GONE, Detroit: Become Human, na moja ya mchezo uliosubiriwa zaidi, The Last Guardian.
Shirika la ABC lilitangaza kuwa, michezo mingi zaidi itafanya kazi na SONY VR, vifaa vitakavyopatikana kwa bei ya kuanzia Dola 399, kufikia mwezi wa 9 mwaka huu. Michezo kama Resident Evil, Final Fanstasy 4 pia itafanya kazi katika vifaa hivi.
Vyanzo : Daily Mail, ABC na Sci-Tech Today