Space X kazini tena, Safari hii wachemka

0
Sambaza

Space X wamekwisha fanya safari kadhaa za roketi na kufanikiwa kuzishusha roketi hizi duniani ili zitumike tena. Jana  walirusha tena roketi nyingine lakini safari hii hawakufanikiwa kuirudisha salama ardhini.

follow url

x

buy propecia 1mg uk Roketi hiyo ikiwa inapaa kutoka ardhini.

Space X safari hii walikuwa wanarusha satelite mbili za mawasiliano za Eutelsat na ABS, baada ya kuzifikisha roketi hizo katika obit yake roketi hiyo ilirudi duniani ila wakati wa kutua katika meli maalumu ilianguka.

Space X walikwisha fanya safari kama hii na kufanikiwa kurudisha roketi katika hali ya usalama mwezi  Mei, Kwa mujibu wa CNN tukio hili lilitegemewa kuwa gumu kidogo kutokana na ukweli kwamba roketi hiyo ilikuwa inaenda anga la mbali hivyo ingerudi na mwendo mkali zaidi.

x

Screenshot ikionesha roketi hii ikianzisha hatua ya pili ya safari yake.

Kila kitu kilikuwa kinaonekana kinaenda sawa mpaka pale ambapo matangazo ya moja kwa moja yalipokatika sekunde chache kabla ya roeketi hiyo kutua katika meli maalumu na kuwaacha waliokuwa wakifuatilia tukio hilo bila ya kujua nini hasa kimetokea.

INAYOHUSIANA  Kilimo kinachotumia teknolojia zaidi

Ingawa sio habari nzuri lakini kushindwa kwa tukio hili hakutarudisha nyuma jitihada za kampuni hii ya mambo ya anga kwakuwa bado wanajaribu njia mbali mbali za kufanikisha kutua roketi salama baada ya kushusha mzigo angani.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.