Space X ya rusha na kisha kuirudisha roketi duniani salama (kwa mara nyingine).

1
Sambaza

Kampuni ya Space X inayojihusisha na mambo ya anga imefanikiwa kwa mara nyingine tena kurusha na kuirudisha roketi duniani ikiwa salama, safari hii tukio hili limefanyika katika kiwanja cha kurushia roketi chenye utajiri wa historia ya mambo ya anga.

Roketi hii iliyopewa jina la Dragon ilirushwa jumapili baada ya tukio hili kushindikana siku ya jumamosi baada ya kutokea tatizo la kiufundi, roketi hii ilikuwa imebeba mzigo wa mahitaji mbalimbali kwaajiri ya kituo cha kimataifa cha anga na ilikuwa na uzito unaopata tani 2.

SOMA PIA:  Siri: Programu ya Apple yaita ambyulensi kumsaidia mtoto

Teknoloji ya kurusha roketi kisha kuirudisha duniani.

Kabla ya hapa roketi zilikuwa zinarushwa angani kisha baada ya kuufikisha mzigo huanguka duniani na haziwezi kutumika tena, Space X ndio kampuni ya kwanza kurusha na kisha kuirudisha roketi duniani kwaajiri ya kutumika tena.

space x

Roketi hiyo ikitua duniani baada ya kurusha mzigo katika anga.

Kwanini tukio hili la mwishoni mwa wiki limeongelewa saana na vyombo vya habari?!

Kwanza ni kwasababu roketi hiyo imerushwa katika kiwanja ambacho kilitumiwa katika misheni za Apollo kurusha roketi, misheni hizi zilikuwa na mchango mkubwa katika utafiti wa anga. Pia hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Space X kurusha roketi kutokea mji wa Florida baada ya ajali iliyotokea mwezi Septemba mwaka jana.

SOMA PIA:  Utafiti: Hizi ndio Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi katika simu za Android

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.
error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com