SPACE X yafanikiwa kutua Roketi katika Meli! #Teknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

SPACE X yafanikiwa kutua Roketi katika Meli! #Teknolojia

1
Sambaza

Hatimaye siku ya Ijumaa Space X wamefanikiwa kutua roketi katika meli baada ya kutumika  kurusha mizigo kwenda katika kituo cha wanaanga wa NASA. Katika mizigo iliyopelekwa katika kituo cha anga pia ni pamoja na aina mpya ya makazi ambayo bado haijatumika angani.

http://cpabod.com/client-letter/

Spx-F9-Landing-Burn

here Space X ni kampuni iliyojikita katika teknolojia ya kurusha roketi, kampuni hii mwaka jana mwishoni iliwekeza pesa nyingi katika kujaribu kuhakikisha kwamba roketi zinarorushwa kupeleka mizigo zinatua salama duniani (badala ya kuanguka baharini kama ilivyokuwa mwanzoni ) ili kutumiwa tena.

kutua roketi katika meli

Picha ikiwa inaonesha jinsi roketi hiyo inavyosimama baada ya kutua katika meli.

Space X walishafanya majaribio kadhaa mwezi Disemba kujaribu kutua roketi katika meli lakini mara zote walishindwa kufanikiwa kwa asilimia mia moja. Ingawa walikwisha fanikiwa kufanya zoezi hili katika nchi kavu kwa majini Ijumaa ndiyo ilikuwa mara ya kwanza wanafanikiwa .

buy finasteride 1mg online Soma zaidi: Space X yashindwa jaribio lake la kutua roketi katika meli.

INAYOHUSIANA  Ijue ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner


Akiongea kwa furaha Elon Musk ambaye ndiye mmiliki wa kampuni hiyo amesema kwamba wanafuraha  kwasababu roketi hiyo haikutoboa meli na imetua salama.

Safari hii ilikuwa muhimu kwa sababu tatu muhimu, kwanza ni kwasababu moja ya mzigo uliokuwa unapelekwa huko ni aina mpya ya makazi ambayo inaenda huko kwa mara ya kwanza, lakini pia hii ilikuwa ndiyo safari ya kwanza ya Space X kupeleka mizigo ya NASA baada ya kusitishwa kwa muda na tatu ni kwamba Space X  waliamua kutumia nafasi hii kujaribu kutua roketi katika meli baada ya kufikisha mzigo kitu ambacho kilifanikiwa.

Kwa kawaida roketi zimekuwa zikitumiwa kupeleka mizigo katika anga na baada ya kufika huko roketi hizi hurudi na kuanguka duniani na ni ngumu kutumika tena maana zinaharibika, Space X walikuwa wanatafuta njia ambayo itawasaidia kurudisha roketi duniani katika hali ya kiusalama na kuweza kutumika tena kitu ambacho kingepunguza gharama za urushaji roketi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.