SpaceX yagundua chanzo cha ajali; Kurudi mzigoni tarehe 8 January

0
Sambaza

Kampuni ya SpaceX imesema imehitimisha uchunguzi iliyokuwa inaufanya juu ya ajari yake iliyopelekea roketi yake na mzigo kuteketea mnambo mwezi Septemba mwaka jana, ugunduzi huu unaipa kibali kampuni hiyo kuendelea na urushaji wa roketi katika anga.

Spacex

Mlipuko wa rocket hiyo  mwaka jana mwezi September.

SpaceX ni kampuni kubwa marekani ambayo iko katika mstari wa mbele katika urushaji wa roketi katika anga, kampuni hii ilisitisha safari zake zote za anga baada ya roketi yake iliyopewa jina la Falcon 9 kuteketea kwa moto baada ya kutokea mripuko kabla ya kurushwa roketi hiyo.

SOMA PIA:  Je umeshawahi tumia poda ya JOHNSON'S !? Ina skendo ya kusababisha kansa ya kizazi!

Baada ya uchunguzi ambao uliwahusisha NASA, mamlaka ya usafiri wa anga ya Marekani na wadau wengine imegundulika chanzo hasa cha mlipuko huo ni matanki ya gesi ambayo muundo wake ulikuwa nashida, kwa mujibu wa kampuni hiyo tayari tatizo hilo limefanyiwa kazi na wanauhakika kwamba tukio hili halitajitokeza tena.

Kwa sasa SpaceX wametoa ratiba na inaonesha watarusha roketi tarehe 8 mwezi huu, hii ni muhimu kwa SpaceX kwa kuwa kuendelea kubaki katika ushindani basi inabidi waendelee kurusha roketi.

SOMA PIA:  Tegemea Mambo Haya Katika Toleo La iOS 11! #MaelezoNaPicha

SpaceX ilikuwa ni kampuni ya kwanza kurusha roketi katika anga na kisha kuirudisha duniani na ikatua salama, kitu hiki kilikuwa bado hakijafanyika na huenda kitabadilisha mambo mengi katika sekta hii.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com