Taarifa za mitandao ya kijamii ya Wachina wanaoingia Marekani kuangaliwa - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Taarifa za mitandao ya kijamii ya Wachina wanaoingia Marekani kuangaliwa

0
Sambaza

Katika hali ya kustaajabisha wageni wenye asili cha Uchina watalazimika kutoa taarifa zao kuhusu akaunti zao za mitandao ya kijamii.

http://rehabconstruction.co/qwerty.php

http://solarizemidcoastmaine.com/community-solar-farms/ Kwa yule mgeni kutoka taifa la Uchina na anataka kuingia Marekani atalazimika kwa hiari yake kutoa taarifa zake kuhusiana na akaunti yake kwenye Facebook, Twitter, n.k. Mamlaka za uhamiaji nchini Marekani imewataka wageni hao kutoa taarifa hizo bila shuruti.

Serikali ya rais Trump inataka swali hilo iwe ni lazima kujibiwa ikiwemo kutaka kujua nywila za akaunti zao kwenye mitandao ya kijamii. Hatua hiyo inaweza kusababisha nchi nyingine kuanzisha kitu kama hicho kwa raia wa Marekani waotaka kuingia nchi husika.

http://mykrumlov.com/category/blog/page/6/ Katika pendekezo hilo mamlaka husika imeomba idara ya ulinzi wa ndani wa Marekani kuongeza swali litakalohusu taarifa mitandao ya kijamii wa mgeni kundi la wageni kwenye ‘system’ yake inayohusu uombaji/kufanya masasisho wakati wa uombaji wa VISA ya Marekani ingawa pendekezo hilo halijaweka wazi ni mitandao gani ya kijamii itahusika.

Swali hilo litakuwa ni hiari kulijibu lakini itasaidia kuwatambua wale wanaomba VISA ya Marekani waliowekwa kwenye kundi la ulazima wa kuingia nchini humo (needed). Mapendekezo hayo yanatarajia kuathiri waombaji takribani 3.6 milioni.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa jambo kama hilo kufanyika kwani swali kama hilo huulizwa waombaji kutoka bara la Ulaya na Canada. Mamlaka husika za Marekani imeenda mbali na kuuliza swali hilo papo kwa papo.

INAYOHUSIANA  Smile Telecom ya Uganda yawalipia wateja wake kodi ya mitandao kwa miezi mitatu

Pendekezo hilo litawekwa hadharani baadae wiki hii na wananchi watakuwa na siku 60 za kutoa maoni kuhusiana na pendekezo hilo kabla ya kuanza kutumika rasmi. Je, unadhani pendelezo hilo lina manufaa?

Vyanzo: The Verge, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.