Katika mahojiano na gazeti la New York Times bilionea Jack Ma ameeleza mpango wake wa kujiuzulu kama Mwenyekiti Mtendaji wa mtandao maarufu wa biashara, Alibaba unaojulikana kama ‘Amazon ya Uchina’.
Jack Ma anatarajia kuachia ngazi nafasi hiyo kuanzia Jumatatu (Sept. 10) na kubaki kuwa mmiliki wa mtandao huo pamoja na kujihusisha katika kutoa elimu ya kusaidia watu wasiojiweza.
Alibaba ni mtandao maarufu na mkubwa nchini Uchina kwa uuzaji wa bidhaa mbalimbali duniani kote. Jack Ma alianzisha mtandao wa Alibaba mwaka 1999 akiwa na mkewe pamoja na wenzie wengine wapatao 19.
Kulingana na taarifa ya gazeti hilo Mkurugenzi Mtendaji wa sasa, Daniel Zhang anatarajiwa kushika nafasi itakayoachwa na Jack Ma.