Takwimu za Tanzania na uhalifu wa kwenye mtandao #Uchambuzi #Ripoti - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Takwimu za Tanzania na uhalifu wa kwenye mtandao #Uchambuzi #Ripoti

2
Sambaza

Tanzania ni nchi changa sana kwenye masuala ya uhalifu wa kwenye mtandao na mara baada mara baada ya kuhudhuria mkutano wa wadau na wana TEHAMA mwishoni mwa mwezi Oktoba 2017 tulifahamu mengi ambayo Tanzania imekumbana nayo katika vita ya kupambana na uhalifu wa kwenye mtandao.

Katika vitu ambavyo Tanzania inasumbukanavyo ingawa si wengi wanaofahamu ni suala zima la udukuzi wa aina mbalimbali pamoja na makosa ya kwenye mtandao hata mara baada ya sheria ya makosa ya kwenye mtandao kuidhinishwa mwaka 2015 bado hali si ya kuridhisha sana.

Lakini vita ya uhalifu wa kwenye mtandao na udukuzi inasabishwa na nini?

Matumizi ya intaneti ndio kiini cha uhalifu wa kimtandao pamoja na udukuzi ulioletwa na maendeleo makubwa kwenye teknolojia iliyopanuka na inayoendelea kupanuka kila siku. see url Tanzania ina watu zaidi ya mil. 7 wanatumia intaneti na zaidi ya watu mil. 40 wanaotumia simu za kiganjani.

Takwimu zinaonyesha kuwa nchini Tazania kuna akaunti hai za kwenye mitandao ya kijamii takribani mil. 3.7. Matumizi ya simu janja yanachangia kwa kiasi kikubwa watu kuwa na akaunti kwenye mitandao ya kijamii; siku hizi chini ya dakika tatu mtu anakuw tayari ameshajiunga na mtandao wa kijamii.

 Hali ya udukuzi nchini Tanzania.

 Kama nchi nyingine zinavyosumbuliwa na suala zima la udukuzi vilevile Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazopingana vikali na udukuzi wa aina yoyote ile. Mwaka 2016, http://yfgroup.ca/category/employees/ Tanzania ilipoteza kiasi cha Tsh. 9.8bn kwa sababu ya uhalifu wa kwenye mtandao.

INAYOHUSIANA  Ijue ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner

Tarehe 4 Okt 2017 akaunti ya Twitter ya TTCL ilidukuliwa. Chuo kikuu Huria Tanzania (OUT) pamoja na chuo kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM) pia ni miongoni mwa taasisi za elimu zilizowahi kudukuliwa ingawa udukuzi huo uliweza kukabiliwa na kuweza kumiliki tena akaunti/wavuti husika.

Ujumbe uliowasilishwa na wadukuzi kama ishara ya tovuti hiyo kudukuliwa.

Katika sehemu ambazo wadukuzi wanafanya uhalifu wao kwa kiasi kikubwa ni upande wa miamala inayofanyika kwa njia ya simu na kwa taarifa Tanzania imepoteza karibu Tsh. 187bn kwa njia ya miamala iliyofanyika kwa njia ya simu.

Uelewa mdogo wa Watanzania unachangia kutojua namna gani ya kuepukana na utapeli wa kwenye mtandao ndio inafanya Tanzania iwe miongoni mwa nchi zinazowindwa sana kwenye masuala ya udukuzi. see url Mwaka 2015 Tanzania ilikuwa moja ya nchi zilizoongoza kwa kudukuliwa.

Takwimu za mikoa iliyoshambuliwa na uhalifu wa kwenye mtandao kwa mwaka 2015.

Ni wazi kwamba Tanzania ina wataalamu wachache wanaofahamu namna gani ya kukabiliana na udukuzi na hii inachangiwa sana na gharama za juu sana kwa kozi zinazohusina na masuala ya usalama wa kwenye mtandao.

Kuna umuhimu wa mamlaka husika kuweza kuliangalia suala hili kwa ukaribu zaidi ili idadi ya wataalamu wa masuala ya udukuzi iongezeke na Watanzania waelimishwe zaidi.

Vyanzo: AIPC na IPP Media

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|