Tanesco & Selcom: Sababu ya Kushindwa Kununua Umeme wa Luku

0
Sambaza

Kama umejaribu kununua umeme katika hizi siku mbili kupitia kwenye baadhi ya wakala au kwenye makampuni ya simu kama Mpesa, Tigo Pesa na ata Airtel Money utakuwa umegundua jambo hilo haliwezekani kwa sasa. Sababu kuu ni kwamba shirika la Tanesco limevunja mkataba na mmoja wa mtoa huduma hiyo ya ununuzi wa Luku, kampuni ya Selcom.

Hali ilivyokuwa:

  • Manunuzi yote ya luku yalikuwa yakifanyika kupitia mitambo ya makampuni mawili, Maxcom na Selcom.
  • Makampuni haya ndiyo yanayowapa wengine kama vile mitandao ya simu na mabenki uwezo wa kununua na kulipia huduma ya umeme -Luku
  • Hivyo mara nyingi pale ulipokuwa unapata shida kununua umeme inakuwa pale ambapo mfumo wa malipo unaotegemea mitambo ya moja ya hizi kampuni mbili unakuwa na hitilafu.
SOMA PIA:  Hizi ndio apps salama zaidi kwa kuchati - ripoti ya Amnesty International, 2016!

Tanesco kupitia amri ya WAZIRI wa Nishati na Madini, George Simbachawene,  na ushauri wa TRA wamevunja mkataba wa uwakala na Kampuni ya Selcom. Sababu kubwa zilizotolewa ni kutokana na mitambo yake ya kuuza LUKU kuwa na matatizo ikiwemo matatizo ya kisheria katika kulipa kodi.

airtel tanzania bando

Sasa utaweza kununua umeme kupitia vituo vya MaxMalipo na vya Luku - Tanesco.

Kwa sasa utaweza kununua umeme kupitia vituo vya MaxMalipo na vya Luku – Tanesco.

Inasemekano kero nyingi za ukosekaji wa huduma ya manunuzi ya LUKU ambayo imekuwa ikitokea hivi karibuni imekuwa ni kutokana na mitambo ya kampuni hii kusumbua.

SOMA PIA:  Ujumbe wa kejeli umekuwa msukumo mkubwa mtu kufanyiwa upasuaji

Je utaweza kununua simu kupitia huduma za simu tena?

Kwa kuwa kabla ya hili kutokea makampuni ya simu na baadhi ya mabenki yalikuwa yanatoa huduma hiyo ya ununuaji wa umeme wa LUKU kupitia mitambo ya Selcom kwa sasa utaendelea kukosa huduma hiyo. Ila kama kutakuwa na uwezekano wa haraka makampuni haya kupata huduma hiyo kupitia mitambo ya Maxcom basi utaweza kupata huduma hiyo mara moja.

Kwa sasa utaendelea kupata huduma hiyo kupitia vituo vya mauzo ya Luku vya Tanesco au sehemu inayouza umeme kupitia huduma ya MaxMalipo. Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia! TeknoKona!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. – Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom

| mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com