Tanzania Ina Mfumo wa Kupata Cheti cha Kuzaliwa kwa Simu

1
Sambaza
Picha Na Milicom Foundation

Picha Na Milicom Foundation

Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye watoto wengi ambao hawajasajiliwa (pdf) ingawa sheria inamtaka kila mtoto anayezaliwa kusajiliwa. Miongoni mwa sababu zinazofanya hali kuwa hivi ni wazazi kukosa elimu ya faida na umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa, gharama za upatikanaji wake na miundombinu mibovu ya usafiri kwenye maeneo ya vijijini ambako huduma za serikali zipo halmashauri. Teknolojia ya simu za mkononi ina uwezo wa kubadili hiyo.

Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Tigo Tanzania na UNICEF wana mfumo unaowapa uwezo wahudumu wa afya kuwasilisha vyeti za kuzaliwa ndani ya siku chache kwa kutumia ujumbe mfupi wa simu za mkononi (SMS). Mfumo huo ulianzishwa mwaka 2013. Mfumo huo tayari upo kwenye mikoa 10, ikiwemo Mbeya na serikali ipo tayari kuueneza kwenye mikoa mingine.

SOMA PIA:  Miaka 30 ya mafaili ya mtindo wa GIF. - Fahamu historia yake!

Taratibu Zake

Mhudumu wa afya anatuma ujumbe mfupi wa SMS ukiwa na jina, jinsia, tarehe ya kuzaliwa na taarifa za familia kwenda kwenye “central database”, ambayo ni mahali maalumu kiteknolijia ya kuhifadhi taarifa nyingi. “Database” hiyo inaratibiwa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ambalo ni asasi ya kiserekali. Ujumbe unapopokelewa na RITA, nyaraka zinazohitajika hutengenezwa moja-kwa-moja (“automated response”) na kuweza kutolewa kwa muhitaji baada muda mfupi. Serikali inatazamia kuutandaza mfumo huu wa kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa simu mahali kote nchini ndani ya miaka 5 ijayo.

SOMA PIA:  Smart TV: Jinsi ya kuzuia isidukuliwe

Tanzania yaangazia Teknolojia

Mfumo huu mpya ni muendelezo wa mpango wa serikali ya Tanzania kutumia teknolojia kukuza maendeleo. Kwa sasa, mtandao wa simu za mkononi umewafikia asilia 73 ya watanzania. Lengo lilopo sasa kuhusu mfumo huu ni kutoa vyeti za kuzaliwa kwa takribani watoto millioni moja kabla ya mwaka 2015 kuisha na kusajili asilimia 90 ya watoto wanaozaliwa ndani ya miaka mitano.

Mtandao wa simu za mkononi umewafikia asilia 73 ya watanzania.

Mtandao wa simu za mkononi umewafikia asilia 73 ya watanzania.

Bila cheti cha kuzaliwa, inakuwa vigumu kwa mtoto kupata huduma za afya, elimu na huduma nyingine za muhimu. Jambo ambalo mfumo huu unajaribu kufanya linatazamwa na wataalamu wengi kuwa hatua nzuri ya kuipa serikali uwezo wa kutoa huduma bora zaidi.

SOMA PIA:  Kampuni yashtakiwa kutokana na Headphones zinazofanya ujasusi kwa watumiaji wake

Angalia video ya kuelezea mfumo huo kutoka asasi ya Milicom (Kwa kiingereza)

Picha Na: Milicom Foundation, Reuters/Afolabi Sotunde

Chanzo: Omar Mohammed. In Tanzania, you can now get your birth certificate by mobile phone.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

1 Comment

  1. Pingback: Tanzania Ina Mfumo wa Kupata Cheti cha Kuzaliwa kwa Simu | Teknolojia

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com