Taylor Swift Anakuja Na Gemu Lake Kwa Kushirikiana Na Glu Mobile!

0
Sambaza

Mwanamuziki wa kimataifa Taylor Swift ana mipango ya kuletagemu la kwenye simu janja mwishoni mwa mwaka huu. Msanii huyo wa mtindo wa Pop atashirikiana na kampuni ya Glu Mobile katika kuandaa mchezo (Gemu) huo.

Gemu hiyo itatoka rasmi mwishoni mwa mwaka 2016. Inaonekana wazi kwamba tuanze kufikiria mafanikio makubwa zaidi ya Taylor Swift katika ulimwengu wa kidigitali. Kumbuka hata katika mtandao msanii huyu anafanya vizuri sana.

Taylor Swift alisema ataungana na Glu Mobile katika kutengeneza Gemu ambalo litakuwa ni bure kabisa kucheza. Ambalo pia litakuwa ni moto wakuotea mbali kwani mtu yeyote angetegemea gemu hilo kuwa nzuri  hata ingekuwa kwa msanii mwingine mkubwa yeyote.

SOMA PIA:  Apps zilizopakuliwa mara nyingi zaidi tangu kutambulishwa kwake #Uchambuzi

Taylor Swift

Taylor Swift ana mashabiki (fans )milioni 74 katika mtandao wa kijamii wa Facebook, Milioni 64.8 Katika Instagram, milioni 70.4 katika Twitter na watu milioni 8 katika katika akaunti yake ya Vevo katika mtandao wa Youtube.

Taylor Swift ana takribani nyimbo milioni 130 ambazo zimeshushwa duniani katika mitandao maarufu na mauzo ya albamu milioni 40. Na kwa sasa albamu yake ya 1989 inagombea tuzo za albamu ya mwaka katika tuzo za Grammy. Pia anagombea vipengele 7 katika tuzo hizo mwaka huu (2016)

SOMA PIA:  Emoji mpya 2017 zinakujia, zifahamu mpya zinazokuja

Kama kawaida Glu Mobel imefanikiwa sana kwa kutengeneza gemu za watu maarufu. Kwa mfano kampuni la Glu limtengenezea Gemu la Kim Kardashian ambalo lilikuja kuwa lenye faida sana. Gemu hilo liliingiza dola za kimarekani milioni 43 kwa miezi yake mitatu tuu ya mwanzo.

Baadhi Ya Magemu Kutoka Glu Mobile

Baadhi Ya Magemu Kutoka Glu Mobile

Gemu hili la Taylor Swift kuna hati hati likawa lipo kama video ya ‘Blad Blood’ ya msanii huyo. Kampuni la Glu limeahidi kuwa litaongeza manjonjo na mbwembwe katika ushirikano na msanii huyo wa kutengeneza gemu hili.

SOMA PIA:  Siri: Programu ya Apple yaita ambyulensi kumsaidia mtoto

Uzuri wa jambo hili ni kwamba, Mwana  dada Taylor Swift hatopata tabu kwani kulingana na network aliyonayo anaweza kulitangaza Gemu hili na likapata watu wengi wa kulicheza (ndani ya muda mchache).

Tuandikie sehemu ya comment hapo chini wewe unahisi nini katika ushirikan huu? Je litafanya vizuri sana na kulipita lile la Kim? Tembelea TeknoKona kila siku kupata habari mpya mpya. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com