Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo Agosti, 7 2018 la kusudio la kusimamisha leseni zilizotolewa kwa MULTICHOICE TANZANIA LIMITED (Dstv) na Simbanet Tanzania Ltd (ZUKU) kwa kushindwa kutekeleza amri halali za TCRA.
Aidha, kusudio la TCRA kwa kampuni hizo mbili ni kushindwa kutekeleza masharti ya leseni ikiwa ni pamoja na kjumuishwa kwa chaneli ambazo zinapaswa kuonyeshwa bure kwenye vifurushi vyao.
Simbanet Tanzania Limited, Multichoice Tanzania Limited, hairuhusiwi kuonyesha chaneli za televisheni zenye leseni za kutazamwa bila malipo kupitia ving’amuzi vyao isipokuwa TBC1 peke yake~TCRA.