TCRA: Tarehe ya kuzimwa simu feki haitasogezwa mbele

0
Sambaza

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imeendelea kusistiza kwamba tarehe ya kuzimwa simu zote feki itaabaki palepale na watu wasitegemee kusogezwa kwa muda. TCRA walitangaza mwaka jana mwishoni kwamba tarehe 16 mwezi wa sita watazima simu zote ambazo ni feki.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi mkuu wa TCRA bwana Yahya Simba amesema kwamba japo kuwa watu wengi wameomba kusogezwa mbele kwa tarehe hiyo lakini mamlaka haitaongeza siku kwa kuwa muda ulio tolewa unatosha.

SOMA PIA:  Nokia 2: Simu janja mpya ya bei nafuu, yenye kukaa na chaji kwa siku mbili

Mamlaka ya mawasiliano wataka watumiaji wote wa simu nchini Tanzania kuhakikisha kwamba wanatumia simu ambazo ni orijino kabla ya tarehe 16 mwezi Juni kwani baada ya hapo mamlaka hiyo ingezima simu zote ambazo sio simu orijino.

airtel ofa kabambe

simu feki tcra

Aidha mamlaka hiyo iliskwisha toa namna ambayo mtumiaji anaweza kuangalia kama simu yake ni orijino ama siyo na Teknokona tulikuletea makala juu ya hilo kama bado hujaisoma SOMA HAPA.

Simu ambazo sio original zina madhara mengi kwa mtumiaji kwa kuwa wakati mwingine zinatengenezwa bila ya kufuata viwango maalumu kama vile madini ya risasi ambayo ni hatari kwa afya za binadamu.

SOMA PIA:  Simu janja ya kwanza kabisa kutoka kampuni ya utengenezaji magemu

Kuzimwa kwa simu feki ifikapo tarehe 16 mwezi June kunaweza kusaidia kupunguza wahalifu wa kimtandao kwa kuwa wahalifu wengi wa kimtandao hutumia simu ambazo sio original ili wasiweze kugundulika.

Teknokona inaendelea kuwashauri wasomaji wake kuhakikisha kama simu zao ni salama ili kuepuka usumbufu utakao jitokeza.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com