Tecno waingia mkataba wa kimatangazo na timu ya Manchester City

0
Sambaza

Inaonekana kampuni ya Tecno Mobile imeamua kuingia kwenye soko la dunia kwa miguu yote miwili na sio majaribio.

Tecno waingia mkataba

Tecno waingia mkataba wa kimatangazo na timu ya Manchester City

Hili limeonekana zaidi baada ya kampuni hiyo ya simu kutoka nchini China kuingia mkataba wa kimatangazo na moja ya timu kubwa nchini Uingereza, Manchester City FC.

Kwa miaka mingi Tecno wamekuwa wakitengeza simu na kuuza kwa bara la Afrika tuu, ni mwezi wa tisa tuu kwenye utambulisho wa toleo la Tecno Phantom 6 ndio kampuni hiyo ilitangaza rasmi kuanza kuuza simu zake duniani kote.

Mkurugenzi Muendeshaji wa Tecno Mobile, Stephen Ha, akiwa na Mkurugenzi Masoko wa City Football Group, baada ya utambulisho rasmi

Bado ni mapema kujua mafanikio yao ya haraka ila baada ya mwaka au miaka miwili tutaweza kujua nafasi yao katika ushindani mkubwa wa soko ulio tawaliwa na makampuni kama vile Apple, Samsung, Huawei na makampuni mengine mengi yenye miaka mingi katika ushindani wa soko la simu la dunia.

SOMA PIA:  Axon M: Simu janja yenye vioo viwili kutoka ZTE

Timu ya Manchester City FC ni moja ya timu inayofanya vizuri katika ligi kuu ya nchini Uingereza na ipo katika mashindano kimataifa ya barani Ulaya, kupitia mkataba huu inaonekana moja kwa moja Tecno watanufaika kuwafikia kwa urahisi mashabiki mbalimbali wa timu hiyo nchini Uingereza na barani Ulaya – na duniani kote.

Soma Pia;

SOMA PIA:  Ifahamu simu ya Moto Z kutoka Lenovo! #Uchambuzi

Je wewe ni mtumiaji wa simu ya Tecno? Tuambia unaonaje dili hili la Tecno kwa Manchester City?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com