Tecno watambulisha Phantom 6 na 6 Plus; Na sasa Kupatikana Duniani kote

0

Kampuni ya utengenezaji simu ya Tecno yatambulisha rasmi simu mpya ya Tecno Phantom 6 na Phantom 6 Plus jijini Dubai. Utambulisho huu pia umekuja sambamba na taarifa rasmi juu ya uamuzi wao wa kuanza kuuza simu zao duniani kote.

Kwa miaka 10 sasa simu za Tecno zilikuwa zinatengenezwa kwa ajili ya soko la Afrika tuu na inaonekana basi wameweza kukua na kutengeneza faida inayowapa nguvu ya kuingiza ushindani katika soko la simu la duniani kote lenye ushindani mkubwa kutoka Samsung, Apple na Huawei.

tecno phantom 6

Uzinduzi huo wa Phantom 6 jijini Dubai ulihusisha pia uzinduzi rasmi wa ofisi zao za Dubai, na tayari wapo katika maandalizi ya kufungua ofisi zingine Amerika ya Kusini, na pia kwenye mataifa ya Asia ya Kusini.

Je kuna nini kipya katika Phantom 6 na 6 Plus?

Bofya kusoma zaidi;

Simu hizi mbili zimekuja vizuri, kusoma sifa zake kiundani bofya kwenye hizo linki hapo juu ila nitakupa utofauti kwa ufupi.

tecno phantom 6 tecno phantom 6 plus

Tecno Phantom 6 inakuja na display ya inchi 5.5 wakati Phnatom 6 Plus inakuja na display ya inchi 6. Simu zote zinakuja na teknolojia ya ulinzi wa display ya Gorilla Glass.

Phantom 6 inakuja na RAM ya GB 3 wakati 6 Plus inakuja na RAM ya GB 4. Phantom 6 inakuja na ujazo wa diski wa GB 32 huku ukiweza kuweka memori kadi ya hadi GB 128, Phantom 6 Plus inakuja na ujazo wa GB 64 lakini hautaweza kutumia memori kadi.

Simu zote mbili zinakubali teknolojia za mawasiliano ya 2G, 3G na 4G LTE.

Kwenye kamera Phantom 6 inakuja na Megapixel 13 huku kamera ya selfi ikiwa megapixel 5, 6Plus inakuja na kamera ya megapixel 20.1 na selfi ya megapixel 8.

Kwenye betri pia kuna tofauti kubwa ambapo Phantom 6 inakuja na betri la mAh 2700 huku 6Plus ikija na betri la kiwango cha mAh 4050.

Vipi unauonaje uamuzi wa Tecno wa kusambaa duniani kote? Na umepokeaje ujio wa simu hizi mbili? Tuambie kwenye comment, tutaendelea kufuatilia ujio wa simu hizi nchini na tutazichambua kwa kina.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com