Tecno Wazindua Simu Mpya Ya Phantom 8!

0
Sambaza

Kampuni ya utengenezaji wa simu ya Tecno imezindua simu yake mpya inayojulikana kwa jina la Phantom 8 ambayo ipo katika muendelezo wa matoleo ya Phantom. Uzinduzi umefanyika huko Dubai.

Phantom 8 inakuja na mambo mazuri kwa watumiaji wa Simu Janja kwa kuwa na kamera mbili za nyuma. Phantom 8 itakuwa na ukubwa wa kioo cha inchi 5.7 chenye full HD. Pia Katika suala la RAM safari hii Tecno wameongeza ukubwa kwa kuwa na RAM ya GB 6.

Muonekano wa mbele wa Tecno Phantom 8

Ujazo wa ndani utakuwa na GB 64 na unaweza kuweka memori kadi mpaka ukubwa wa 2TB. Simu ya mwisho ya Tecno ya familia ya Phantom ilikuwa ni Phantom 6 na Phantom 6 Plus iliyotolewa mwaka jana.

SOMA PIA:  Apple yatoa MacBook Pro (2017) iliyo bora zaidi

Kwanini ni Tecno Phantom 8 na si Tecno Phantom 7?

Unaweza kujiuliza mbona hawakutoa Phantom 7 na badala yake wameenda Phantom 8? Sababu kubwa iliyoelezwa ni kwamba kampuni imevuka ubora ambao huenda ungekuwepo kwenye Phantom 7. Hivyo basi simu imeboreshwa zaidi na hivyo toleo hilo ikabidi kurukwa kwenda katika toleo bora kabisa (Phantom 8)

.Kwa upande wa Betri litakuwa na ujazo wa ukubwa wa 3500mAh ambapo ni tofauti na toleo la Phantom 6 lilikuwa na ujazo wa 4000mAh.

SOMA PIA:  Je simu za mkononi zinasababisha kansa ya ubongo? Utafiti mpya waja na majibu

Sifa kamili za Phantom 8 ni kama ifuatavyo:

Teknolojia ya mawasiliano:

GSM: GSM 850 / 900 / 1800 / 1900
WCDMA:B1/B2/B3/B5/B8
4G: Ndio
4G Band: FDD-LTE:B1/B2/B3/B4/B5/B7/B8/B20/B28A;
TDD-LTE:B38/B40
SIM: inatumia line mbili za simu

Mfumo Endeshi:
Android 7.0 Nougat

Uhifadhi:

RAM: 6GB na Ujazo wa ndani (Storage): 64GB. Eneo la memori kadi (External Storage): Unaweza kuweka mpaka memori ya ukubwa wa 2TB.

Prosesa:

Octa-Core Processor (MediaTek MT6557CD)

Kamera:

Kamera ya nyuma (Rear): zipo mbili, moja itakuwa na 12MP na nyingine 13MP. Kamera ya mbele (Selfie): 20MP megapixel

SOMA PIA:  Ujenzi wa Darubini kubwa zaidi duniani waanza.

Betri:

ujazo wa 3500mAh

Simu hiyo ambayo bado haijawekwa wazi ni kiasi gani itauzwa lakini kwa maswali zaidi juu ya hili unaweza kuwasilina na Tecno kupitia mitandao yao ya kijamii.

Kama unavyojua simu za kutoka Tecno zilivyo, huwa zinakuwa na sifa za ubora wa hali ya juu kabisa lakini vile vile zinakuwa zinauzwa kwa bei ambayo mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu, ukilinganisha na simu zingine nyingi.

Aidha pia haijawekwa wazi ni lini itaanza kuuzwa lakini taarifa za awali zinaelezwa muda mfupi ujao zitapatikana katika nchi za Nigeria, Kenya, Tanzania, Ghana, Indonesia, UAE, Uganda, Ethiopia, Iran, na India.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com