Tecno yauza kwa asilimia 7 zaidi katika soko la Misri 2017 - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Tecno yauza kwa asilimia 7 zaidi katika soko la Misri 2017

0
Sambaza

Kampuni ya Transsion Holdings inayozalisha simu za Tecno na nyinginezo zilizopo chini ya kampuni huyo imeanza kupata mafanikio katika soko la nchini Misri kwa simu zake kuongezeka kwa asilimia 7 ya soko la simu nchini humo mpaka kufkia mwishoni mwa mwaka 2017.

go to link

Katika soko la Misri, Tecno inasema ni moja ya soko gumu sana ikilinganishwa na masoko mengine kwa sababu kuna bidhaa nyingi za kiwango cha juu katika biashara ya simu ingawa kampuni hiyo inaamini kuwa mauzo ya simu zake yataongezeka kwa mwaka huu, 2018.

Tecno imeingia ushirikiano na kampuni mbili za mawasiliano nchini Misri; Telecom Egypt na Orange Egypt hivyo kuwa na matarajio makubwa ya simu zake kuwafikia wananchi wengi wa nchi hiyo.

yauza kwa asilimia 7

Mauzo ya Transsion Holdings yameimarika: Bidhaa mbalibali zikiongozwa na Tecno zimeonekana kupendwa zaidi kati ya mwaka 2016 na 2017.

Hata hivyo, Tecno inasema watalizingatia soko la Misri kwani ni muhimu zaidi katika Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. http://themaatrust.org/info.php K enter wa mujibu wa kampuni ya StatCounter, kampuni inayoongoza kwa kuuza simu nyingi zaidi Misri ni Samsung, Huawei, iPhone na Lenovo. Simu zingine zinazochangia katika soko la simu, Misri ni Tecno, Infinix, HTC na Nokia.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Wamiliki/Viongozi wa kundi kuamua nani atume ujumbe

Hivi karibuni Tecno ilizindua simu 4 huko Lagos nchini Nigeria za Camon X, Camon X Pro, F1, F2, na Pop. Tecno imeendelea kujidhatiti katika soko la bara la Afrika.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.