Kampuni ya Transsion Holdings ambayo ndio wazalishaji wa simu za Tecno Apr 5 walizindua simu janja mpya ya Tecno Camon X katika tukio lililofanyika jijini Lagos, Nigeria.
Sambamba na Tecno Camon X pia simu zingine zilizozinduliwa siku hiyo ni Tecno Camon X Pro, Tecno F1, Tecno F2 na Tecno POP1. Tecno Camon X na X Pro zinatofauti katika diski uhifadhi na RAM vingine vyote vinafanana.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Waziri wa Mawasiliano wa Nigeria, Bw. Abdur-Raheem Adebayo Shittu ambaye aliishukuru kampuni ya Transsion Holding kwa kutoa ajira 3,000 kwa Wanaigeria na aliwaambia ni muhimu kwa kampuni hiyo kuwekeza zaidi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Mapema katika mkutano na waandishi wa habari Meneja mkuu wa Transsion Holdings, Bw. Stephen Ha alisema Camon X inakuja na kipengele cha picha bora na hakika kwa wapenzi wa Selfie itawafurahisha sana.
Aidha, Tecno walitangaza kuingia ushirika na kampuni ya Google ili kuimarisha uzalishaji wa simu nyingi zitakazokuwa na bei nafuu kwa watumiaji wengi barani Afrika.
Sifa za TECNO Camon X
Aina ya kioo: IPS LCD
Ukubwa wa kioo: 6 inchi (18:9)Mfumo endeshi: Android 8.1 Oreo
Aina ya Prosesa: MediaTek Helio P23
Ukubwa Prosesa: Octa-core 2.0GHzUkubwa wa RAM: 3GB (4GB kwa toleo la Pro )
Uhifadhi wa ndani: 16GB (64GB kwa toleo la Pro)
Memori kadi ya nje: Ukubwa mpaka 128GBTeknoloji mawasiliano: 4G LTE
SIM: Laini mbiliKamera ya nyuma: 16 MP, Ring flash
Kamera ya mbele: 24 MP, dual-flashUkubwa Betri: 3750mAh
Aina ya Betri: Li-Po
Rangi ya simu: Midnight Black
Ulinzi: Fingerprint (rear-mounted), Face ID
Mbali na Tecno Camon X pia Tecno ilitangaza uzinduzi wa simu zake za familia ya F ambazo ni Tecno F1, Tecno F2 na Tecno POP1 (a.k.a Tecno F3). Simu hizi zote zitakuwa na mfumo endeshi wa Android Oreo (Go edition).
Karibu zote zinafanana sifa zake kuu na tofauti ni kwenye kamera ambapo Tecno POP1 itakuwa na kamera ya mbele yenye megapixel 5 na ya nyuma megapixel 8.
Sifa za Tecno F1, F2 na Tecno POP1
Mfumo endeshi: Android Oreo (Go edition)
Ukubwa wa kioo: inchi 5.7, 18:9
Kamera ya nyuma: 8MP
Kamera ya mbele: 2MP selfie camera (5MP kwa POP1)
Prosesa: 1.3GHz quad-core MT6735
Ukubwa Betri: 3000mAh
Ukubwa wa RAM: 1GB RAM
Uhifadhi wa ndani: 16GB
Ulinzi: Fingerprint sensor