TeknoKona Inakuleta Karibu Na: SanDisk Connect Wireless Stick (USB Flash Drive)! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

TeknoKona Inakuleta Karibu Na: SanDisk Connect Wireless Stick (USB Flash Drive)!

0
Sambaza

Inaweza ikawa ni miujiza kwako kama ni mgeni wa teknolojia, lakini kama ni mzoefu wa mambo haya utasema —nlijua tuu!— Kampuni ya SanDisk  licha ya kuwa kampuni ambayo inasifika sana kwa kutengeneza vifaa vyenye uwezo

wa kuhifadhi kumbukumbu (memory) kama vile memori kadi na flash.  Bado ni kampuni ambalo linatoa vitu vyenye hadhi ya teknolojia ya kisasa. USB Diski hii vile vile inatumia chaji ya kujitegemea yaani bila hata ya umeme inafanya kazi (Kama ikichajiwa) kwa muda wa masaa manne na nusu tangia ichajiwe.

USB Ya SanDisk

USB Diski Ya SanDisk

http://secondhelpingsatlanta.org/chefs-table-nights-maya/ MIUJIZA NDANI YA USB DISKI HII

  •  Pata mafaili yako bila kutumia waya au hata internet
  •  Bila kutumia waya  waweza ‘save’ na kutembelea mafaili yako
  •  Unaweza ‘share’ mafaili yako hata kwa marafiki zako
  •  Unaweza uka ‘stream’ video mpaka kwa vifaa vitatu kwa wakati mmoja (lakini USB Diski hiyo iwe karibu tuu Mfano nyuma ya siti)
  • Uwezo wa ku ‘back up’ picha zako katika ‘camera roll’ automatiki
  • USB Diski hii inauwezo wa ku ‘save’ kuhamisha na pia kuonesha mafaili katika kifaa chochote chenye WiFi hii inajumuisha iOS na Android, Amazon Fire tablets, Macs, na kompyuta. Pia unaweza chomeka katika kompyuta yako ili kutuma na kuhamisha mafaili kiurahisi zaidi.
INAYOHUSIANA  Ijue simu mpya kutoka Motorola ya Moto Z3 Play

App ambayo itakusaidi kutumia USB Diski hii unaweza kuiipata katika  App Store, Google Play store, na Amazon Appstore na ni bure kabisa

Pia kifaa kinapatikana katika uwezo wa 16GB, 32GB, 64GB, and 128GB kutoka Amazon, BestBuy.com, na SanDisk.com

san

http://ashleyannlaz.com/?p=1148 Angalia Video Fupi Inayoelezea USB DIski hii

[iframe id=”https://www.youtube.com/embed/TaCjquOZPPI” align=”center”]

SanDisk wanakuambia ”Kizazi kipya cha uhifadhi hakihitaji waya au intaneti ili kujipatia taarifa (mfaili) zako”. Tuambie USB Diski hii unaionaje,, vipi ukilinganisha na zile za kawaida?. Tuandikie sehemu ya comment hapo chini na pia Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKonaDotCom kila siku. TeknoKona Tupo Nawe!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply