TeknoKona Mwaka 2015: Fahamu Makala 10 Yaliyosomwa Zaidi Mwaka 2015 - TeknoKona Teknolojia Tanzania

TeknoKona Mwaka 2015: Fahamu Makala 10 Yaliyosomwa Zaidi Mwaka 2015

0
Sambaza

Leo tunakuletea orodha ya makala 10 yaliyosomwa zaidi kwa mwaka 2015.

Katika orodha hii kuna makala mengine ni ya mwaka 2014 lakini bado yameingia kwenye orodha hii kutokana ya kuendelea kusomwa zaidi kwa mwaka 2015.

Orodha imeshikiliwa zaidi na makala za uchambuzi wa simu pamoja na makala za maujanja – yaani tulizokufundisha kufanya mambo mbalimbali.

http://saintjohnsbeltsville.org/visit-us/directions/ TANGAZO;

Pata Offer ukinunua vifurushi kabambe kutoka SMARTcha Tsh 999 tu, Pata Dk 25 za kupiga mitandao yote na Unlimited SMS. Piga *149*00# kujiunga. SMART- let’s talk!

Posted by Smart Tanzania on Wednesday, December 30, 2015

1. Ifahamu Tecno Phantom Z Mini, Uwezo wa Juu kwa Bei ya Kawaida

Makala hii inahusu uchambuzi wa simu ya Tecno Phantom Z Mini, inashikilia namba moja kwa mwaka huu kwa kusomwa na watu wengi zaidi kwa mwaka 2015.

Makala ya iliandikwa tarehe 27 mwezi wa kwanza mwaka 2015. Unaweza kusoma uchambuzi mzima hapa -> http://teknokona.com/2015/01/27/tecno-phantom-z-v7-bei-simu/ 

2. Uchambuzi: Ifahamu Tecno Boom J7, Bei na Uwezo Wake!

Makala hii inahusu uchambuzi wa simu ya Tecno Boom J7, inashikilia namba mbili katika orodha ya makala zilizosomwa zaidi mwaka 2015.

Iliandikwa tarehe 21 mwezi wa tano mwaka 2015. Unaweza kusoma uchambuzi mzima hapa -> http://teknokona.com/2015/05/21/uchambuzi-tecno-boom-j7-bei-na-uwezo-wake/

INAYOHUSIANA  Waliopewa dhamana ya kusimamia mifumo ya TEHAMA serikalini waonywa na kutakiwa kuzingatia weledi kazini

3. Epuka Simu Feki: Baini Simu Halisi Kirahisi

Moja ya makala ya miaka ya nyuma iliyofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2015. Ni makala inayokupa njia rahisi za kutambua kama simu unayonunua ni ‘original’ au imetumia muonekano wa simu unayoiitaji na hivyo kukudanganya – zinafahamika kama ‘clone’.

Hii ni makala ya mwaka 2014, iliandikwa tarehe 2 mwezi wa saba. Unaweza kusoma makala nzima hapa -> http://teknokona.com/2014/09/02/ufanye-nini-kubaini-simu-halisi/

4. Mambo 6 Yasiyo ya Kweli Kuhusu Kuchaji Simu

Ni makala inayokuelezea ukweli kuhusu mambo 6 ambayo unaweza ukawa umeshayasikia yanayohusisha masuala ya kuchaji simu. Hii ni pamoja na vitu vya kufanya na kutofanya vinavyohusisha jinsi tunavyochaji simu au tableti zetu.

Hii ni makala iliyoandikwa tarehe 28 mwezi wa kwanza, 2015. Soma makala nzima hapa -> http://teknokona.com/2015/01/28/mambo-6-yasiyo-ya-kweli-kuchaji-simu/

5. Jinsi Ya Kufufua Mafaili Yaliyofutwa Katika Simu/Kompyuta!

Hii ni makala inayokuonesha njia kadhaa za kukuwezesha kuyapata tena mafaili uliyofuta kwa bahati mbaya, iwe kwenye simu au kompyuta.

Makala hii iliandikwa tarehe 16 mwezi wa pili 2015, unaweza isoma makala nzima nzima hapa -> http://teknokona.com/2015/02/16/jinsi-ya-kufufua-mafaili-yaliyofutwa-katika-simukompyuta/

6. Fahamu kwa Nini Mtandao Mpya wa Simu wa Viettel Unaogopeka! Wapewa Tuhuma za Kuhujumu Miundombinu ya Wengine.

Hii ni makala inayoongelea ujio wa kampuni mpya ya simu ya Viettel, ambayo inatumia jina la ‘brand’ – Halotel… Kabla ya ata kampuni hii mpya ya simu kuanza huduma tayari kulikuwa na malalamiko kutoka makampuni mengine ya simu. Kupitia makala hii tuliweza kukuonesha kwa nini kampuni hii ya simu iliianza kuogopwa mapema na baadhi ya wapinzani wake katika biashara hiyo.

INAYOHUSIANA  Ukuaji wa teknolojia katika kamera za kwenye simu

Makala iliandikwa tarehe 30 mwezi wa sita, mwaka 2015. Unaweza kusoma makala nzima hapa -> http://teknokona.com/2015/06/30/fahamu-kwa-nini-mtandao-wa-mpya-wa-simu-wa-viettel-unaogopeka-wapewa-tuhuma-za-kuhujumu-miundombinu-ya-wengine/

7. Mambo ya Kufanya Kuepuka Kulipukiwa na Betri za Simu!

Uwepo wa betri na chaja zilizo chini ya kiwango kumeweka usalama wa watu wengi kwenye hali hatarishi. Kupitia makala hii tumekupa dondoo kadhaa za kuhakikisha unakuwa salama.

Makala hii iliandikwa tarehe 4 mwezi wa sita, 2015. Unaweza kusoma makala nzima hapa -> http://teknokona.com/2015/06/04/mambo-ya-kufanya-kuepuka-kulipukiwa-na-betri-za-simu/

8. Fahamu Tofauti Kuu Kati ya Teknolojia za 2G, 3G, 4G n.k

Ujio wa mitandao ya simu kama Smile na Smart kumefanya na mitandao mingine mingi ya simu kuanza kujitutumua katika eneo la huduma ya intaneti kwa kutumia teknolojia ya 4G. Makala hii inakuelezea kwa urahisi historia na utofauti wa teknolojia mbalimbali za huduma ya mawasiliano na intaneti.

Makala hii iliandikwa tarehe 27 mwezi wa nne, 2015. Unaweza kusoma makala nzima hapa -> http://teknokona.com/2015/04/27/fahamu-tofauti-kuu-kati-ya-teknolojia-za-2g-3g-4g-n-k/

INAYOHUSIANA  Clickfarms: Wauza Likes, Shares, na Comments wakamatwa nchini Thailand

9. Mbinu Ambazo Huenda Huzijui Katika Google PlayStore!

Kuna mambo mengi mazuri yanayopatikana kupitia huduma ya Google Play na programu endeshaji ya Android. Kupitia makala hii unaweza fahamu mengi unayoweza fanya kwenye simu yako, hii ni pamoja na jinsi kufuatilia simu iliyopotea au kuibiwa n.k.

Makala hii ni ya mwaka 2014, tarehe 14 mwezi wa kumi na moja. Unaweza kusoma makala nzima hapa -> http://teknokona.com/2014/11/14/mbinu-ambazo-huenda-huzijui-katika-google-playstore/

10. Jinsi Kuzuia Mtu Kujua Kama Umesoma Ujumbe ktk WhatsApp

Hakika watu wengi wanapenda uhuru wa kuweza kumjibu mtu pale wanapotaka wao na sio kwa sababu whatsapp wamemwambia mtu aliyetuma ujumbe huo ya kwembe mpokeaji ameshausoma. Makala hii inakuonesha jinsi gani ya kuzuia mtu aliyepokea ujumbe kupata alama za kuonesha wewe umesoma ujumbe wake.

Makala hii iliandikwa tarehe 24 mwezi wa sita, mwaka 2015. Kusoma makala hii bofya hapa -> http://teknokona.com/2015/06/24/jinsi-kuzuia-mtu-kujua-kama-umesoma-ujumbe-ktk-whatsapp/

Hiyo ndiyo orodha ya makala yaliyosomwa zaidi katika mtandao wako namba moja wa habari za teknolojia kwa lugha ya kiswahili.

Tuambie ni makala gani uliipenda zaidi mwaka 2015 kutoka kwetu? Kumbuka pia kuungana nasi kwenye mitandao ya kijamii, bofya -> Twitter, Facebook &Instagram

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply