Nokia wawafungulia mashtaka Apple nchini Ujerumani na Marekani wakidai kampuni hiyo imekuwa ikitumia teknolojia zake mbalimbali bila kulipia.
Nokia wamefikia hatua ya kufungua mashtaka baada ya kuona mazungumzo yao na Apple kuhusu malipo ambayo wanastahili kuyapata kutofanikiwa kwa miaka kadhaa sasa.
Nokia ni waanzilishi wa teknolojia mbalimbali za kimawasiliano na wana hati miliki ya teknolojia hizo. Katika taarifa za mahakama juu ya kesi waliyofungua dhidi ya Apple wamejumuisha utumiaji wa teknolojia 32 ambazo zinagusa maeneo kama vile ya ‘display’, antena, uchezaji video katika simu na nyingine nyingi.
Mara kwa mara makampuni makubwa hasa ya utengenezaji simu yamekuwa yakishitakiana sana ili kuweza kupata fidia ya kipesa juu ya utumiaji wa teknolojia mbalimbali ambazo wao ndio wamezianzisha.
Soma Pia;