Teknolojia ya 3D kutumiwa kuunda nywele za binadamu

0
Sambaza

Tumezoea kuona teknolojia ya 3D katika magemu au tukienda kuangalia sinema au hata majumbani kwetu kwa wale wenye Tv’s ambazo zina teknolojia ya 3D watakuwa si wageni kwa hili lakini teknolojia hiyo inaonekana kwenda mbali zaidi.

Kampuni moja nchini Ufaransa imesema kwamba teknolojia sawa na ile inayotumiwa kupiga chapa vitu vya uhalisia, 3D, huenda ikatumiwa kuunda nywele za binadamu na hivyo kufaa wenye upara. Nywele hizo baadaye zitaweza kupandikizwa kwenye watu waliopoteza nywele.

Teknolojia ya 3D kutumika kutengeneza nywele na nywele hizo kuwa msaada kwa wenye vipara.

Teknolojia ya 3D kutumika kutengeneza nywele na nywele hizo kuwa msaada kwa wenye vipara.

Kampuni ya L’Oreal inashirikiana na kampuni ya kupiga chapa viumbe hai ya Poietis, ambayo imeunda teknolojia ya kupiga chapa kwa kutumia laser ambayo inaweza kuunda sehemu za seli za viumbe.

Mitambo inayotumiwa kuunda seli za viumbe

Mitambo inayotumiwa kuunda seli za viumbe

Vinyweleo vya nywele havijawahi kuundwa kwa njia hii awali lakini kampuni hizo mbili zinatarajia kwamba zitaweza kustawisha teknolojia na kuwezesha kuundwa kwa vinyweleo hivyo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

SOMA PIA:  Nova Launcher yapakuliwa mara milioni 50 mpaka sasa

Hata hivyo, shirika moja linaloangazia watu wanaopoteza nywele limesema bado ni mapema mno kwa watu kuanza kushangilia. L’Oreal tayari hutumia ngozi iliyoundwa kwa teknolojia ya 3D kufanyia utafiti bidhaa za kutumiwa kwenye ngozi.

 Vyanzo: BBC

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com