Teknolojia ya Face ID kwenye iPhone X yaendelea kukosolewa

0
Sambaza

Kitengo cha teknolojia cha Marekani kimeikosoa simu mpya ya iPhone X  na kusema kuwa ufunguaji wa simu hiyo kwa kutumia uso pekee (teknolojia ya Face ID) sio sahihi hasa kwa mapacha na watoto wa chini ya umri wa miaka 13.

Kwa mujibu wa habari, kitengo cha teknolojia nchini Marekani kimeitaka kampuni ya Apple kuhakikisha teknolojia hiyo haisimami peke yake tuu kufungua simu hiyo, bali itumike sambamba na njia zingine.

Teknolojia ya Face ID kwenye iPhone X yaendelea kukosolewa

Teknolojia ya Face ID kwenye iPhone X

Vilevile kitengo hicho kimesema kuwa baadhi ya sura za watoto zinakuwa hazijakua na kutambulika vizuri na kutokana na sababu hiyo itakuwa ni vigumu kwao kuitegemea teknolojia hiyo.

SOMA PIA:  Undani wa Nokia 8 na kupata masasisho ya Android 8.0

Ripoti zilizotolewa na kitengo hicho cha teknolojia cha Marekani zimeonyesha kuwa mapacha au watu wanaofanana watapata shida katika utumiaji wa simu hiyo. Inawezekana ikawa rahisi sana kwa watu waliofanana sura kuweza kufungua simu ya mtu mwingine.

Ila bado Apple wanasema utumiaji wa teknolojia ya 3D katika Face ID unahakikisha kwa kiasi kikubwa njia hii ni salama kuzidi zingine zinazotumia utambuzi wa sura. Ila bado wengi wanaona teknolojia hii inaitaji maboresho ili kuifanya iwe salama zaidi.

Mwezi uliopita kampuni ya Apple ilikubali kasoro ya tatizo la sauti kwenye iPhone 8 na kuahidi kulishughulikia.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com