Teknolojia ya FaceID kuruhusu uso mmoja tu kusajiliwa

0
Sambaza

iPhone X ambayo tangu kuzinduliwa kwake (Sept 12) imekuwa gumzo hasa hasa kwa sababu simu hiyo imekuja na teknolojia tofauti ambayo ni mbadala wa TouchID.

Kwa utafiti wetu TeknoKona ni kwamba iPhone X imekuwa na mapokezi tofauti tofauti kulingana na watu ambao wameshaijaribu teknolojia hiyo mpya kutoka Apple. Maswali mengi yamekuwa yakihusiana na FaceID ambayo Apple imeweka kitu cha kipekee sana kwenye teknolojia hiyo mpya kwenye iPhone X.

Tofauti ya kipekee kwenye teknolojia ya FaceID.

Kwa yeyote yule ambaye anatumia simu janja aina ya iPhone kuanzia iPhone 5s mpaka 8 utakubaliana na mimi kwamba wakati wa kusajili alama yako ya kidole una uwezo wa kusajili alama za vidole za  watu wengine wanne (hii inamaanisha na wao pia watakuwa na uwezo wa kufungua simu yako kwa kuweka alama yao ya kidole).

Kwenye FaceID inaruhusu uso wa mtu mmja tu kusajiliwa na hivyo kuifanya teknolojia hiyo kuwa ya tofauti kabisa kulinganisha na TouchID.

Ni uso wa mtu mmoja tu ndio utakaoweza kusajiliwa kwenye teknolojia ya FaceID iliyo kwenye iPhone X.

Wakati wa uzinduzi wa simu janja ya iPhone X maswali kadha wa kadha yaliulizwa na mojawapo likiwa “Itakuaje simu hiyo (iPhone X) itakapoporwa na kibaka na mtu kuamriwa kuondoa lock?“. Jibu lake likawa Iwapo hutoikodolea macho simu yako basi haitofunguka  pia kama ukiboneza vibonyezeo vilivyopo upande wa kushoto na kulia wa iPhone X basi simu hiyo itandoa kwa muda FaceID“.

Jambo la FaceID kuruhusu uso wa mtu mmoja tu kusajiliwa limeonekana kuwa kama kikwazo kwa kiasi fulani hasa kwa wale ambao wamezoea kuruhusu mtu zaidi ya mmoja kuwa na uwezo wa kufungua simu.

SOMA PIA:  Kampuni yashtakiwa kutokana na Headphones zinazofanya ujasusi kwa watumiaji wake

Apple hawajasema iwapo kama wataruhusu uso zaidi ya mmoja kusajiliwa kwenye teknolojia ya FaceID kwa huko mbeleni. Wewe msomaji wetu unadhani Apple wapo sahihi kwa kuruhu uso mmoja tu kusajiliwa kwenye FaceID?

Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com