Teknolojia ya Li-Fi katika ulimwengu wa intaneti! Li-Fi ni nini?

0
Sambaza

Kwa miaka mingi teknolojia ya Wi-Fi imekuwa ikitumika katika kuwezesha taasisi mbalimbali, majumbani, maofisini kuweza kupata huduma ya intaneti inayotumia mawimbi ya redio kuweza kupata huduma ya intaneti.

Teknolojia ya Li-Fi iligunduliwa mwaka 2011 na mwanazuoni aitwaye Prof. Harald Hass ambaye aliizungumzia teknolojia ya Li-Fi katika onyesho linajulikana kama TED Talk na hatimaye mwaka 2012 teknolojia ya Li-Fi ilizinduliwa rasmi.

Li-Fi ni nini?

Li-Fi (Light Fidelity) ni teknolojia mpya na ya kisasa zaidi inayotumia mwanga wa taa (LED Lights) kusafirisha mawimbi na hatimaye kuweza kupata huduma ya intaneti. source Teknolojia hii ni tofauti na ile ya Wi-Fi ambayo inasafirisha data kwa kutumia mawimbi ya redio kuweza kupata intaneti.

li-fi

Teknolojia ya Li-Fi ni uwezo wa kusafirisha data mara 10 mpaka 50 kulinganisha na Wi-Fi.

Prof. Harald Hass aliona mapungufu usafirishaji wa data kwa kutumia mawimbi ya redio ndio alipoamua kutafuta mbadala wa Wi-Fi na kuja na teknolojia ya kufafirisha data kwa kutumia taa za LED.

Li-Fi inafanyaje kazi?

Li-Fi inafanya kazi kwa kutumia taa za LED zikiwashwa ndio zinakuwa zinasafirisha data kwenda kwenye kompyuta/tableti au kifaa chochote kinachoweza kutumia intaneti.

Kifaa maalum ambacho kina sensor kina uwezo wa kupokea mawimbi yanayosafirishwa kwa njia ya mwanga na kisha kuwezesha kupata huduma ya intaneti.

Kifaa maalum ambacho kina sensor kina uwezo wa kupokea mawimbi yanayosafirishwa kwa njia ya mwanga na kisha kuwezesha kupata huduma ya intaneti.

  follow Kifaa hicho kina uwezo wa kuunganisha kifaa zaidi ya kimoja kutoka kwenye mawimbi yanayosafirishwa na taa mojawapo na kuhamia kwenye taa nyingine bila kuathiri usafirishwaji wa data.

INAYOHUSIANA  Njia rahisi ya kutuma kitu kupitia intaneti

Faida za kutumia teknolojia ya Li-Fi.

  • Li-Fi inasafirisha kiasi kikubwa cha data ndani ya muda mfupi sana ambapo ni mara 50 zaidi ya uwezo wa teknolojia ya Wi-Fi.
  • Teknolojia ya Li-Fi haipiti kwenye ukuta hivyo kufanya mtumiaji kutokuwa na hofu ya mtu mwingine ambaye yupo mbali na sehemu alipo kipata huduma huduma ya intaneti kutoka kwake.
  • Kasi ya kupakuwa na kutuma kitu mtandaoni ni 40Mbs (Megabytes 40 kwa sekunde) kifaa kikiwa katika umabli wa mita 9 mpaka 10.
  • Li-Fi inatumia teknolojia ya taa za LED hivyo wingi wa taa za LED utawezesha kasi zaidi pale unapotumia huduma ya intaneti.
  • Kwa kutumia teknolojia ya Li-Fi unaweza kuwa na watu wanaotumia Li-Fi katika eneo moja.
INAYOHUSIANA  Uchina: Watumiaji wa intaneti wafikia milioni 800

Teknolojia ya Li-Fi kuna uvumi kuwa iPhones ikaacha kutumia teknolojia ya Wi-Fi na kuhamia kwenye teknolojia ya Li-Fi katika iPhones. Je, una lipi la kusema kuhusiana na Li-Fi?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia FacebookTwitterInstagramYouTubeTelegram na Google Plus

Vyanzo: TechWorld, Digital Trends

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.