Pengine unaweza shangaa gemu kwenye kamera ya Snapchat inawezakana vipi lakini kwa kutumia teknolojia ya AR hili linawezekana.
Kumbuka magemu kama Pokemon Go yanatumia teknolojia hii, sasa gemu hii ya Snapchat iko hivi yenyewe inakuwezesha kutumia kamera katika App ya Snapchat kuweza kutafuta majini/mashetani katika mazingira yanayokuzunguka……
Sio Kweli ni gemu tuu hahaha, Gemu hilo jipya linakwenda kwa jina la Ghost Phone, hadithi yake ni kwamba kuna binti anaitwa Lisa na wewe utakua unatumia simu yake ili kujua mahali alipo, pia simu hiyo ina uwezo wa kutambua majini/mashetani
Itakubidi upitie vikwazo vingi kama vile kujua neno siri la simu hiyo, kushindana na majini/mashetani hao n.k
Kwa kifupi itakubidi ufanye mambo mengi sana ili kujua nini kimempata huyo Lisa…..
Jinsi Ya Kucheza.
- Fungua Snapchat.
- Fungua sehemu ya kamera ya kurekodi video au kupiga.
- Nenda katika menu ya Lens.
- Ingia katika sehemu ya “Explore” upande wa kulia chini katika skrini
- Tafuta “Ghost Phone.”
- Ingia katika Ghost Phone. Utaona picha ya simu janja yenye kiulizo.
Mpaka hapo nadhani na wewe utakua umeshajua jinsi ya kilifikia gemu hili na kuanza kulicheza, uzuri wake litakua linatumia mazingira yale yale ambayo yamekuzunguka kiuhalisia kabisa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la commet? Je umeshacheza gemu hii? Kama bado hebu fanya hivyo alafu nipe mrejesho hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.