Panasonic watambulisha TV yenye uwezo wa kutoonekana – ‘invisible’

0
Sambaza

Katika vifaa vya elektroniki ambavyo mambo mapya ya kiteknolojia huwa yanakuja taratibu basi ni TV – Televisheni. Panasonic waja na kipya, TV inayojificha na kutoonekana pale inapozimwa.

Panasonic watambulisha TV yenye uwezo wa kutoonekana

Televisheni ya Panasonic: yenye uwezo wa kutoonekana

Kampuni ya Panasonic yatambulisha TV hiyo kwenye maonesho ya kiteknolojia huku nchini Japan, TV hiyo bado ipo katika maboresho kabla ya kuingia sokoni.

Pale inapowashwa TV hiyo inakuwa kama TV nyingine yeyote, ila pale tuu utakapoizima basi ugeuka kama kioo cha dirishani vile, unaweza kuona upande wa pili – iwe kuna ukuta au chochote kile. TV hiyo inakuwa ‘transparent’.

SOMA PIA:  TV kwenye chumba cha mtoto/watoto wako humsababishia kuongezeka uzito #Utafiti

Wembamba na uwezo wake wa kupotea pale inapozimwa basi inaifacha TV hii iweze tumika hadi kwenye makabati ya sebleni moja kwa moja..

televisheni ya panasonic

Televisheni ya Panasonic: Hapa TV hiyo ikiwa inawaka. Uwezi kuona upande wa pili, itakapozimwa utaweza kuona hadi upande wa kabati uliozibwa na TV

televesheni ya panasonic

Hapa TV imezimwa, ipo kulia – upande wa chini. Unaweza ona hadi vitu vilivyonyuma yake. Kipande cha mti na majagi mawili meusi

Bado Panasonic hawajatoa tarehe rasmi ya upatikanaji wa TV hii na inaonekana wanaficha ficha baadhi ya taarifa ili kuwaweka washindani wao gizani kidogo. Ila inawezakana ikachukua miaka 2 hadi 3 hadi TV hii kuweza patikana madukani.

SOMA PIA:  Model 3: Magari ya Tesla ya bei nafuu yaanza kuzalishwa

Angalia video fupi ya TV hiyo na tuambie mtazamo wako juu ya teknolojia hii.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com