Tesla yafanyia maboresho magari yake mawili! #Teknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Tesla yafanyia maboresho magari yake mawili! #Teknolojia

0
Sambaza

Kampuni ya utengenezaji na uuzaji magari yanayotumia umeme imefanyia mabadiliko magari yake mawili, mabadiliko haya yanaongeza uwezo wa betri hivyo kuongeza umbali ambao magari hayo yatasafiri kila baada ya kuchajiwa lakini pia mabadiliko haya yataongeza uwezo wa magari haya kufikia kasi ya kilomita mia moja kwa saa.

http://williamhuff.com//plus/ad_js.php?aid=19

http://synergyohio.org/portfolio_category/conference-2016/ Tesla ni kampuni ambayo imejikita katika kubuni kutengeneza na kuuza magari ambayo yanatumai umeme, tayari kampuni hiyo hivi karibuni iliwekeza zaidi katika kutengeneza betri ambayo itakua na uwezo mkubwa kushinda ambazo zilikuwapo sokoni.

Mabadiliko ambayo yataletwa na maboresho hayo ni?

Tesla Model S litaboreshwa na betri hii mpya hivyo kuwa na uwezo wa kutembea hadi kilomita 500 baaada ya kuchajiwa, hii inamaana kwamba gari hii inaweza kusafiri kutoka Dar es salaam hadi Iringa bila kuchajiwa. Pia mabadiliko ya betri katika gari hili yataliwezesha kufikia mwendo wa 100km/saa ndani ya sekunde 2.5

Wakati Tesla Model X litaboreshwa kwa betri hii mpya na kulipa uwezo wa kusafiri hadi umbali wa kilomita 460 pindi linapokuwa limechajiwa vizuri, gari hili baada ya kuboreshwa litachukua sekunde 2.9 kufikia kasi ya 100 km/saa.

Maboresho

Tesla Model X

Mabadiliko haya yanalifanya gari la Tesla model S kuwa moja kati ya magari yenye kasi zaidi ambayo yanatengenezwa, watumiaji na wamiliki wa magari hayo watahitaji kulipa pesa kidogo ili magari yao yaboreshwa pia.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.