´╗┐ Tetesi: Gharama ya iPhone 8 kuwa zaidi ya sh. 2.2M - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Tetesi: Gharama ya iPhone 8 kuwa zaidi ya sh. 2.2M

0
Sambaza

Apple ambao wanasifika kwa kutoa bidhaa zilizo katika kiwango cha juu katika ubora lakini pia kwa bidhaa ghali zaidi kulinganisha na makampuni mengine yaliyo katika ushindani wa kibiashara kama Apple.

click Tangu mwaka 2007 Apple walipotoa iPhone yao ya kwanza na kuendelea mpaka hivi leo ambapo toleo la hivi karibuni likiwa ni iPhone 7 na iPhone 7 plus lakini tangu walipoanza biashara ya simu janja hazijawahi kuuzwa kwa gharama ya juu sana kama uvumi kuhusu bei ya iPhone 8.

Ni ongezeko la 54% kwa gharama ya iPhone 8 ukilinganisha na bei ya iPhone 7 inayoanzia $649 (zaidi ya Tsh. 1.4m).

Kwanini iPhone 8 kuwa ghali sana?

http://casinogamblingchamp.com/2016/01/the-long-march/ Jibu la swali hili ni rahisi na kupitia tovuti mbalimbali imeelezwa ni kwa sababu ya gharama iliyotumika kutengeneza simu hiyo huku simu hiyo pia kuwa katika mkunjo (curved) wa kipekee (katika kila pembe ya simu) na utakubaliana nasi kuwa simu janja nyingi za hivi karibu zimekuwa katika mfumo wa mikunjo.

INAYOHUSIANA  Kifaa cha kupima malaria bila ya damu chaundwa nchini Uganda

where to buy Levetiracetam Kama ulitegemea kuwa iPhone 8 itaanziwa katika ujazo hifadhi wa GB 32 sahau kuhusu hilo kwani inaaminika iPhone 8 itakuwa na diski uhifadhi wa kuanzia GB 64 ambapo hakuna iPhone 7 ya ujazo wa GB 64.

gharama ya iphone 8

Muonekano iphone 8 inavyotegemewa kuwa.

iPhone 8 pia itakuwa na ulinzi madhubuti wa kuweza kutambua sura ya mtu kama namna mojawapo ya kuifanya simu hiyo kuwa salama. Na katika uzinduzi huo ambao unategemewa kuwa wa kipekee sana huku Apple wakianzimisha miaka 10 tangu simu yao ya kwanza kuzinduliwa.

Matoleo ya iPhone 7s na iPhone 7s Plus yanategemewa kuzindulwa pamoja na iPhone 8 huku bei zake zikiwa chini kidogo tofauti na bei ya iPhone 8. Baadhi ya sifa za iPhone 8 ni kutokuwa na kitufe cha nyumbani, muundo wake wa nyuma wote kuwa wa kioo na teknolojia ya kuchaji bila waya.

Samsung Galaxy Note 8 ndio simu janja zaidi kati ya simu za hivi karibuni lakini kama ulikuwa hujui Hungary ndio nchi ambayo inauza iPhone 7 kwa gharama ya juu sana. Je, unajipanga ili uweze kununua iPhone 8 mara tu itakapotoka? Tupe maoni yako.

Vyanzo: Telegraph, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.