Simu mpya za iPhone bado hazijatoka ni mpaka baadae mwaka huu lakini tayari kuna picha zilizovuja zikidaiwa kwamba ndio iPhone mpya zitakazozinduliwa miezi michache ijayo.
Ni wazi kwamba Apple ingependa kutofautisha kidogo muonekano wa iPhone (hasa kwenye uwekaji wa kamera zake) zijazo na zile ambazo tayari zimeshatoka. Kuna tofauti ya uwekaji wa kamera kwa simu moja na nyingine. Vioo vya simu zote vinaelezwa vitakuwa na teknolojia ya OLED.
Simu zinazodaiwa kuwa na mabadiliko ni iPhone X Plus na iPhone SE ambapo zinaelezwa kuwa na urefu wa inchi 6.1 na 6.5 kwenye kioo.
Kingine kinachoelezwa kwa simu hizo mpya za iPhone ni kwamba zitakuja na laini mbili kulingana mahitaji ya wateja wake wengi. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa simu za iPhone kuwa na laini mbili; zimezoeleka ni simu zenye laini moja tu.