Tigo na Huawei waungana Katika Huawei Y360

0
Sambaza

Katika kile kinachoonyesha ni kujipanga vyema, kampuni nguli za mawasiliano nchini Huawei na Tigo wameungana kukukufikishia huduma kwa gharama nafuu na haraka zaidi.

Tigo na Huawei wameungana kukuletea simu za mkononi aina ya Huawei Y360 ambazo zitakua zikiuzwa katika maduka ya Tigo nchi nzima.

huawei y360 tigo

Katika kujua watanzania wamelipokeaje hili, nilitembelea maduka kadhaa ya Tigo jijini Dar es Salaam kuzungmza na wateja wao.

Aboubakar Msami mkazi wa Temeke anasema

‘Ni simu nzuri ya kipekee, bei yake ni nafuu na zaidi unarudishiwa pesa hiyo kama vifurushi kwa miezi sita. Nadhani ushirikiano huu wa makampuni uwepo mara kwa mara ili kutunufaisha zaidi’

Nae Antony Shirima anayejishughulisha na uuzaji na utangenezaji wa simu Kariakoo jijini Dar es Salaam alikua na haya ya kusema.

SOMA PIA:  Jelly: Simu janja ndogo zaidi, ya kutosha kiganjani inayokuja na mfumo wa 4G

‘Niliposikia wanauza hii simu 160,000 nilihisi ni kama utani fulani, huwezi kupata smartphone yenye Android 4.4.2, kamera megapixel 5, ya mbele 2 na kioo cha inchi nne kwa bei hiyo labda ziwe zile za watu wenye macho madogo’

huawei y360 specs

Nilimuuliza pia kuhusu ubora wake kwa mtuamiji . Alikua na haya ya kusema

‘Hii simu ni nzuri, CPU yake ni Quad-core 1.2 GHz Cortex-A7 ambayo inaifanya kuwa na kasi sana, pia internal memory yake ya 4GB inakufanya uweze kuitumia bila hata kuweka memory card ya ziada.’

Na je vipi kuhusu kuuzwa kwenye maduka ya Tigo? Hili alilionaje?

SOMA PIA:  Picha za Samsung Galaxy S9 na S9 Plus Zavuja

‘Nadhani ni jambo jema, kwanza kwa sababu Tigo wana maduka nchi nzima hivyo ni rahisi kwa kila mtu kuweza kuipata bila shida, jambo la pili ni kuwa inakuwa ikitoa uhakika zaidi kwa mnunuzi, siku hizi kuna simu feki nyingi sasa ukinunua kwenye maduka ya Tigo unakua na uhakika umenunua bidhaa salama kwani unapata na warranty’

 Je umeshanunua simu hii? Tuambie ulichopemba zaidi kwenye Huawei Y360.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com