TiGo nayo mchakatoni kuingia katika soko la hisa. #Tanzania - TeknoKona Teknolojia Tanzania

TiGo nayo mchakatoni kuingia katika soko la hisa. #Tanzania

0
Sambaza

Baada ya Vodacom kuwa ya kwanza kuingia katika soko la hisa, kampuni ya TiGo imeanzisha mchakato kwa ajiri ya kujiandikisha katika soko la hisa la Dar es salaam zikiwa zimebakia siku chache ili kufikia tarehe ya mwisho ambayo makapuni ya simu yalipewa yawe yamekamilisha  zoezi hili.

TiGo

buy apo prednisone Serikali iliiboresha sheria ambayo ilipitishwa na bunge mwezi Juni ambayo kimsingi inayataka makampuni ya simu kuuza asilimia 25 ya hisa zao kwa umma, jambo hili hata hivyo lilipingwa na umoja wa watoa huduma wa simu kwa kudai kwamba kulazimishwa kujiorodhesha katika soko la hisa ni kinyume na sera za biashara huria.

Diego Gutierrez ambaye ndiye mkurugenzi mtendaji wa TiGo anasema wa wanayofuraha kuanza rasmi mchakato ambao utawawezesha wateja, wafanyakazi na umma wa waTanzania kumiliki hisa za kampuni hiyo.

INAYOHUSIANA  TCRA kuinyang'anya leseni StarTimes

Zipo faida nyingi kwa wanaomiliki hisa za makampuni hivyo wewe kama msomaji sio jambo baya ukaiunga mkono serikali kwa kununua hisa pindi zitakapoanza kuuzwa. SOMA hapa kujua faida za kumiliki hisa za makampuni mbalimbali

Tunategemea hadi mwakani mwezi wa sita makampuni mengi ya mitandao ya simu yatakuwa yamekwisha jiunga katika soko la hisa Dar es salaam kama ambavyo yanatakiwa na sheria.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.