Tim Cook wa Apple asema “Najivunia Kuwa Shoga”

0
Sambaza

tim-cook-apple-ceoCEO – Mkurugenzi mkuu wa kampuni mashuhuri ya vifaa vya elekroniki ya Apple, Bwana Tim Cook amejitangaza kuwa ni shoga!

Bwana Cook amejitangaza rasmi kupitia makala aliyoandika katika mtandao wa BusinessWeek  wiki hii, masaa machache tu yaliyopita. Watu wengi washawahi kuelezea wasi wasi wao kuwa CEO huyo anaweza kuwa ni shoga lakini hii ni mara ya kwanza yeye mwenyewe kulielezea jambo hilo.

Katika makala hiyo Bwana Cook amesema kama ‘kusikia ya kwamba CEO wa kampuni kubwa kama Apple ni shoga kutawasaidia wengine waliokwenye hali hiyo kujikubali na kutosita kujitokeza basi ameona inathamani ya yeye kujitangaza’.

SOMA PIA:  App Store: Apple waiondoa app ya Telegram kwenye soko lake la Apps

Inasemekana wafanyakazi wengi wa kampuni hiyo ya Apple tayari walikuwa wanafahamu ya kuwa Bwana Cook ni shoga, hakuwaficha na amesema anafurahi kwani utamaduni wa Apple ni mzuri na usio tenga watu kutokana na tofauti zao.

Tim Cook akiwa na Steve Jobs

Tim Cook akiwa na Steve Jobs

Je suala hili litaathiri mtazamo wako kwake na kwa kampuni hiyo?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com