Kusafisha simu? Hii ni 'Toilet Paper' kwa ajili ya simu janja yako ????????

Kusafisha simu? Wajapani waja na ‘Toilet Paper’ kwa ajili ya simu yako ????????

1
Sambaza

Je unafahamu ya kwamba simu yako inavijidudu vingi zaidi kuliko vilivyo kwenye kiti cha choo? ???????? Kama hufahamu basi fahamu sasa.

toilet paper ya simu

Suala hili ndilo limetumiwa na mtandao mkubwa wa huduma za intaneti nchini Japan ambao wameamua kuweka toilet paper kwa ajili ya simu janja kwenye vyoo mbalimbali katika moja ya kiwanja cha ndege maarufu huko nchini Japan.

get link Kampuni hiyo ya simu, Docomo, imeweka vidubwasha 86 vya kutolea toilet paper hizo katika vyoo mbalimbali katika kiwanja cha ndege cha Narita.

Wazo kuu la kuja na toilet paper hizo ni data tuliyoitaja juu inayoonesha ya kwamba simu za mkononi zinavijidudu (germs) mara tano zaidi ukilinganisha na idadi ya vijidudu kama hivyo vinavyopatikana katika eneo la kukalia katika vyoo vya kukalia.

INAYOHUSIANA  VPN ni nini? Fahamu app 3 za bure za Huduma ya VPN

Pia katika vikaratasi hivyo kuna http://silverspoonthaiandsushi.com/miami-lakes/?_escaped_fragment_=/menus/25577/categories/68554/items/653213 ujumbe wa kibiashara ambapo wanatangaza ofa mbalimbali za intaneti wanazozitoa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye viwanja vya ndege.

Zinakuja na ofa mbalimbali za huduma zao

Chooni ni moja ya sehemu ambazo Japan inasifika sana kwa kupafanya kuwa sehemu spesheli sana. Je ushasikia kuhusu vyoo vyao vyenye teknolojia ya kukusafisha vyenyewe? Soma hapa – Fahamu Vyoo Janja vya Nchini Japani 

http://amariussen.com/tag/affiliate-marketing/ Vipi wewe unaonaje hili wazo lao hili ambalo kwa kiasi kikubwa linaonekana linafaida kubwa kimatangazo pia?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |