WhatsApp yaongeza aina za herufi na rangi katika Status kwa matoleo ya Android na iOS

0
Sambaza

Toleo jipya la WhatsApp laanza kupatikana. WhatsApp imetangaza kufanya maboresho ya programu yake pendwa kwa kuweka kipengele kipya ambacho kitamuwezesha mtumiaji wake kutumia aina ya Fonts(herufi) mbalimbali azitakazo.

Kipengele hicho kipya kitakuwa katika sehemu ya kuweka Status ambapo mtumiaji ataweza kuweka background ya rangi yoyote aipendayo na kisha kuandika chochote akipendacho kwa aina ya muandiko aupendao.

Toleo jipya la WhatsApp

Toleo jipya la WhatsApp: Namba 1 ni Emoj. Namba 2 ni aina ya Fonts. Namba tatu ni Rangi

Aina ya herufi za namna tano kwa sasa ndio pekee zinazopatikana pamoja na rangi 22.

SOMA PIA:  Apple yatetea uamuzi wake kuondoa App za VPN China

Kwa mujibu wa WhatsApp maboresho haya yanapatikana kwa matoleo yote ya Android na iOS. Ili kupata mabadiliko hayo ni lazima ufanye Update kwa WhatsApp yako.

  • Kuwezesha zoezi hilo, kwanza fungua whatsApp yako, angalia juu na ufungue Status.
  • Ukishafungua kwa chini upande wa kulia utaona kama alama ya kalamu na utaifungua.

Hapo utakuwa umeingia kwenye uwanja wa kuandika Status yako na kuchagua muandiko uupendao na rangi za Background uzipendazo. Maboresho haya yanafanana na yale ya Facebook.

SOMA PIA:  Skype yaingia mkataba na Paypal; sasa watumiaji wataweza kutuma pesa.

Pia kwa wale wanaotumia WhatsApp Web (kwenye kompyuta) kwa sasa wataweza badilisha Status moja kwa moja.

Kumbuka kila baada ya masaa 24 Status itajiondoa na hivyo kulazimika kuiweka tena au kuweka mpya.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com